Habari za Punde

Mgombea Ubunge wa CCM jimbo la Ziwani aahidi kusimamia haki za watu wenye ulemavu

Na Masanja Mabula –Pemba .
 MGOMBEA ubunge wa jimbo la Ziwani kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Mohammed Othman Omar amesema kuwa iwapo wananchi wa jimbo hilo watamwamini na kumchagua kuwa mbunge atasimamia kupatikana haki za watu wenye ulemavu .
Amesema kuwa watu wenye ulemavu wanakosa haki zao za msingi ikiwemo ya kupiga kura kutokana na kukosa fursa ya kujindikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kunasababishwa na kushindwa kupata visaidizi ambavyo vitawawezesha kuzifikia huduma hiyo .
Mgombea huyo ambaye ni mwanachama wa Jumuiya ya watu wenye ulemavu ameyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ambapo pia ametupa lawama kwa viongozi wa majimbo kwa kuwajali walemavu wakati wanapoomba  kura .
Amefahamisha kwamba iwapo atachaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo ataunda kamati ya kushughulikia matatizo ya jimbo hususani kero na changamoto za watu wenye ulemavu pamoja na kutatfuta suluhisho lake .
“Wapo watu wenye ulemavu ambao hawashiriki zoezi la kupiga kura kwani hawakuandikisha , walikosa nyenzo za kufikia kituo cha kuandikisha , naomba tu niwaeleze wananchi wa jimbo la Ziwani kwamba kipaombele change cha kwanza ni kutatua kero za watu wenye ulemavu ”alifahamisha .
Aliongeza kwamba “Nikichaguliwa nitaunda kamati ya kushughulikia kero za wananchi ndani ya Jimbo , na hii itakuwa na wajumbe wawili wawili kutoka kila shehia za jimbo zima ”aliongeza Mohammed Othamn Omar .
Kuhusu changamoto kutoka kwa  wagombea wa vyama vyengine , amesema kuwa amejipanga kukabiliana nazo , kwani atayatumia majukwaa ya kampeni kuelezea vipaombele vyake na jinsi alivyojiandaa kuwaletea maendeleo wananchi .
“Ni kweli zipo changamoto kutoka kwa wagombea wa vyama vyengine , lakini kama nilivyowaomba wanachama wa chama changu  kunipitisha , vilem vile nitawafika wagombea wenzangu kuwaomba kura kwani kauli mbiu yangu ni maendeleo kwanza vyama badaye”alifahamisha .
Katika kampeni zake ameahidi kuwatumia wakalimani kwa ajili ya kutoa tasfiri kwa viziwi ili nao waweze kufahamu sera na kufanya maamuzi tarehe 25 mwezi Oktoba .
Amesema kuwa amekusudia   kuwawekea wakalimani  viziw ambao watoa tafsiri ya sera za wagombea pamoja na ilani ya chama na kwamba hali hiyo itawawezesha kutambua alichokusudia kuwafanyia .
Awena Khamis Rashid katibu wa Jumuiya ya maabilo Pemba ameeleza kwamba iwapo hapatakuwepo na wakalimani kwenye mikutano ya kampeni , huenda  viziwi wakachaguaa kiongozi kwa kuangalia sura yake kutokana na kutokuwepo watu wa kukalimanai sera zao .
“Sisi ambao tunajamaa viziwi tunapata shida kuwafahamisha kinachozungumzwa majukwaani  , kwani baadhi yao huenda wakachagua kiongozi kwa kuangalia sura yake kwani sera za wagombea hawazielewi  , hii inasababishwa na kutokuwepo na wakalimani ”alieleza.
Naye mashavu juma mabrouk katibu kwa ajili ya jumuiya ya watu wenye ulemavau wa akili mkoa wa kusini pemb a amesema kuwa watu wenye ulemavu hususani viziwi  wabakosa haki yao kidemokrasia kutokana kukosekana kwa wakalimani kwenye mikutano ya kampeni .
 Ni vyema viongozi wa vyama vya siasa kuhakikisha kwamba wanakuwa na wakalimani kwenye mikutano yao ya kampeni ili kuwawezesha viziwi kushiriki uchaguzi ambapo Jumuiya ya watu wenye ulemavu imesema kuwa iko tayari kutoa wakalimani iwaapo watahitajika .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.