Habari za Punde

Popo wa Pemba hatarini kutoweka

Na Masanja Mabula –Pemba .

JAMII imetakiwa  kuandaa mikakati madhubuti ya kuwalinda popo wa Pemba dhidi ya watu wanaowawinda kwa ajili ya kitoweyo  , ili kuzuia  wanyama hao ambao ni wadau wakubwa wa mazingira wasitoweke .
Kutoweka kwa wanyama hao kunaweza pia kusababisha kukosekana kwa fedha za kigeni ambazo Taifa linazipata kutokana na wageni wanaokuja kutalii na kuwaona wanyama hao adimu  ambao wahapatikani popote isopokuwa  Kisiwa cha Pemba .
Hayo yamesemwa na Katibu wa Jumuiya ya Kuhifadhi Popo wa Pemba iliyoko Kidike Wilaya ya Wete , Kombo Khamis wakati akizuzngumza na mwandishi wa habari na kuishauri jamii kuhakikisha inaunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Jumuiya hiyo kuwalinda Popo  wa Pemba ili wasitoweke .
Amefahamisha kwamba jumuiya hiyo imepanga  kufungua klabu za kuhifadhi Popo katika maeneo yote ambayo wanyama hao wamehamia  .
 Amesema kuwa awali Jumuiya hiyo ilipanga kufungua Klabu hizo mapema mwaka jana , lakini mpango huo ulishindikana kutokana na ukata wa fedha , ambapo waliendelea  kutoa elimu kwa wananchi kuwalinda Popo .
 “Mipango ya Jumuiya ni kifungua Klabu za kuhifadhi Popo wa Pemba ili wasitoweke , lakini ilishindikana kutokana na ukata wa fedha , kwa sasa tunaendelea kuwaelimisha wananchi wa maeneo ambayo wanyama hawa wamehamia nili wasiendelee kuwindwa na kuliwa ”alifahamisha Kombo .
Naye Mohammed Said Omar wa Makangake akizungumza na mwandishi wa habari hizi kutoweka kwa Popo hao ni hasara kwao na Taifa kwa ujumla kwani licha ya kutokuwa na Klabu ya akuwahifadhi wanawaingia kipato kutokana na wageni wanaokuja kutembea wakitoka kwenye hoteli za kitalii .
Amesema kuwa mbali na Popo hao kuwa ni chanzo cha mapato pia ni sehemu za kusambaza misitu kutoka eneo moja na jengine  na kushauri walindwe na wasiliwe .
“Napata fedha japo kuwa ni kidogo , naamini kwamba wakiwekewa mazingira mazuri kipato kitaongezeka naomba kila mmoja ashiriki kuwahifadhi na tusiwawinde kwa ajili ya kitoweyo na pia tufahamu kwamba hawa ni chanzo cha kusambaza misitu ”alifahamisha .
Kwa upande wake Mick Martin mtalii kutoka Sweeden ameishauri Serikali kuunga mokono Juhudi za Jumuiya ya kuwahifadhi Popo wa Pemba kutokana na kuwa na faida na umuhimu kubwa katika suala la mazingira  .
Mick ambaye alifikia katika Hoteli ya Manta Resort amesema kwamba ameridhishwa na historia aliyopata katika Kituo cha Kidike juu ya faida wa Popo wa Pemba na kusema kuwa akirejea nchini Sweeden atawahamisha Raia wa nchi hiyo kuja kuwatembea maeneo yanayohifadhiwa Popo hao .
“Nimesoma mengi pale Kidike , nitayachukua na hizi picha nitazipeleka Sweeden na nitaenda kuwashawishi wenzangu kuja kuwaona  wanyama hao , nimewapenda na ni ajira nzuri kwa vijana ”alieleza .

Iwapo jamii itaandaa utaratibu wa kuanzia klabu za kuwahifadhi Popo wa Pemba itakuwa ni sehemu ya ajira kwao kutokana wanyama hao kuwa ni kivutio kikubwa cha watalii kutokana na kwamba hawaonekani sehemu nyingine duniani isipokuwa Kisiwa cha Pemba pekee.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.