Mgombea Urais wa ACT Mhe Khamis Iddi Lila akiwasili katika viwanja vya Afisi ya Tume ya Uchaguzi ziliko katika hoteli ya Bwawani Zanzibar kwa ajili ya kurejesha famu yake ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT.
Mgombea Urais kupitia Chama cha ACT Mhe Khamis Iddi Lila akiwa na mkoba wake wa fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar akishindikizwa na Viongozi wa Chama hicho wakiwasili katika Afisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC bwawani Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT Mhe Khamis Iddi Lila akiwa na Viongozi wa Chama hicho wakati wa kurejesha Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar.
Wanachama wa Chama cha ACT wakiwa katika ukumbi wa Tume wakimshindikiza Mgombea wao wa Urais wa Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo.
Mgombea Urais kupitia Chama cha ACT Mhe Khamis Iddi Lila akimkabidhi Fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe. Jecha.S,Jecha alipofika Afisi za Tume zilioko hoteli ya Bwawani Zanzibar kushoto Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Salum Kassin Ali.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT Mhe Khamis Iddi Lila akikabidhi fedha kwa ajili ya malipo ya fomu ya Urais shiliongi milioni mbili kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe. Jecha.S.Jecha wakati wa kurejesha fomu katika Afisi za Tume ya Uchaguzi zilioko katika hoteli ya Bwawani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Mhe Jecha,SJecha akisaini fomu za mgombea wa Chama cha ACT baada ya kuzipokea na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Ndg Salum Kassim Ali akihakiki fomu hizo wakati wa kukabidhiwa Tume na Mgombea.
Mgombea Urais wa Chama cha ACT Mhe Khamis Iddi Lila akitoa shukrani zake kwa Tume ya Uchaguzi baada ya kurejesha fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT na kuwataka Wananchi kusubiri matunda yake kama atapata ridhaa za kucgaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar.
Mgombea Urais kupitia Chama cha ACT Mhe. Khamis Iddi Lila akitoka Afisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC baada ya kurejesha fomu za kugombea nafasi hiyo ya Urais wa Zanzibar.
Sisi Z'bar mwaka huu hatuna changamoto kubwa ya siasa, ndio maana mpaka 'vyama uchwara' vinafanya maigizo, kazi ipo kwa wenzetu Bara, sio siri, MBUYU utatikiswa kweli kweli!
ReplyDeleteSera zimekua haziuziki sasa, watu ni ushabik, ushabik,ushabik, hivyo vyombo vya khabari ndio usiseme utadhani vimenunuliwa na LOWASSA na serikali ya ccm imeshindwa kuvidhibiti!
Sasa yale aliyoyasema KINANA kwamba ndani ya ccm kuna watu mchana ccm usiku vyama vingine ni dhahiri na ccm wameshindwa kuwachukulia hatua mapema sasa hali ni mbaya!
Hata baadhi ya wale waliokua wakitamani mabadiliko sasa wameanza kuogopa, wameanza kujiuliza Tanzania bila ya ccm na ukawa ambao hawajajipanga itakuaje?