Habari za Punde

Mgombea wa Urais Kupitia Chama cha Jahazi Asilia. Arejesha Fomu ya Urais Tume ya Uchaguzi.


Mgombea Urais kupitia Chama cha Jahazi Asilia Mhe Kassim Bakari Ali akiwasili katika viwanja vya Afisi ya Tume bwawani hoteli kwa ajili ya kurejesha fomu ya Urais wa Zanzibar. 
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Jahazi Asilia akionesha mkoba uliokuwa na Fomu zake za kugombea Urais wa Zanzibar akizikabidhi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.

Mgombea Urais wa Chama cha Jahazi Asilia akionesha fedha kabla ya kumkabidhi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
Mgombea Urais kupitia Chama cha Jahazi Asilia Mhe Kassim Bakari Ali akikabidhi fedha za fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar shilingi milioni mbili kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha.S.Jecha.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha,S,Jecha akisaini fomu ya Urais wa Chama cha Jahazi Asilia baada ya kukabidhi Afisi za Tume ya Uchaguzi bwawani hoteli mchana huu.
Mgombea Urais kupitia Chama cha Jahazi Asilia Mhe Kassim Bakari Ali akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali walioko katika Afisi za Tume bwawani Zanzibar baada ya zoezi la kurejesha fomu kukamilika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.