Nyumba ya Makaazi ya Askari wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Micheweni Pemba ambalo lina uwezo wea kuchukua familia kumi kwa wakati mmoja.
Makamu wa
Pili wa rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiondosha kitambaa, kuashiria
kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba ya kulala askari Polisi wilaya ya
Micheweni Pemba, ambayo inajengwa kwa ushirikiano kati ya wananchi na Jeshi la
Polisi,
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiwahutubia Wananchi na Askari wa Jeshi la Polisi Pemba wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la nyumba ya makaazi ya Polisi Wilaya ya Micheweni Pemba.
Mkuu wa
Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe: Omar Khamis Othman akimkaribisha Makamu wa pili wa
rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi
la nyumba Polisi wilaya ya Micheweni, yenye vyumba kumi
Kamanda wa
Polisi Wilaya ya Micheweni Pemba, Fakih Mohamed Yussuf akisoma risala ya ujenzi
wa nyumba ya kulala aksari Polisi inayojengwa kwa pamoja na Jeshi hilo na
wananchi, katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi uliofanywa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.
Viongozi wa
Jeshi la Polisi wakimsikiliza Makamu wa Pili wa rais Mhe: Balozi Seif Iddi,
mara baada ya kuweka jiwe la msingi la nyumba za kulala askari Polisi wilaya ya
Micheweni Pemba.
Baadhi ya Wananachi na Viongozi wa Chama na Serikali wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la nyumba za
kulala askari Polisi wilaya ya Micheweni Pemba
No comments:
Post a Comment