Habari za Punde

NGOs ya Tanzania Yanyakuliwa Tunzo ya Umoja wa Mataifa.



Na MwandishiMaalum,   New York
Mtandao wa Kijamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania ( MJUMITA) ni kati ya Asasi   21 ambazo jana ( jumatatu) zimetangazwa kuwa washindi wa Tuzo ya Ikweta (Equator Prize )  kwa mwaka 2015.

Tuzo hiyo ya Ikwete hutolewa na Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kushirikia na wadau mbalimbali wanaofadhili tuzo hiyo. Kila NGO iliyoshinda Tuzo hiyo inanyakua kitita cha dola 10,000 za Kimarekani.

Ushindiwa MJUMITA pamoja na  NGOs nyingine  20 ulitangazwa na Mkuu wa UNDP Bi.Helen Clark  katika mkutano wake  na wawakilishi wa Muungano wa Waandishi wa Habari wa Umoja wa Mataifa.

Wawakilishi wa  NGOs hizo 21 watapokea Tuzo zao mwezi Desemba wakati wa Mkutano wa Kimataifa utakaojadili mabadiliko ya Tabia nchi ( COP21) utakofanyika Paris, Ufaransa.

MJUMITA  ni mtandao wenye wanachama katika vijiji 450 vilivyopo katika Wilaya 23 za Tanzania na hujishughulisha na utunzaji wa misitu, kuwasaidia wanavijiji kupata hati za kimila za kumiliki ardhi, kutatua migogoro inayohusisha masuala ya ardhi na kubuni miradi ya matumizi sahihi ya ardhi pamoja na raslimali za misitu.

Zaidi  ya watu 500,000 wamenufaika na huduma zinazotolewa na  MJUMITA
Akizungumza wakati wa kuwatangaza washindi hao Bi Helen Clark,aliyefuatana na  Bi. Christiana Figueres a nayeshughulikia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na Bw. Alec Baldwin ambaye n imcheza sinema maarufu na mwanaharakati wa mazingira.


Amesema kuwa NGOs hizo ambazo zinajihusisha Zaidi na utunzaji wa mazingira, kupambana na umaskini ,utunzaji wa ardhi na matumizi endelevu ya ardhi na misitu wamedhihirisha kwamba wanalo jambo la kuifundisha Jumuiya ya Kimataifa.

Akaongeza kwamba Zaidi ya washiriki 100 waliingia katika shindano hilo lakini  21 ndio walioibuka kidedea, huku akisisitiza kila NGOs  zilizoibuka mshindi inahadhi ya aina yake yenye funzo Jumuiya ya Kimataifa.

Akasema kupitia kazi nzuri zinazofanywa na asasi za kijamii pasipo kutumia  gharama kubwa au teknolojia za hali ya juu imedhihirika kwamba kuna juhudi ambazo zinatoa matokeo na watu wengi hasa maskini wanasaidiana na hali yao ya maisha inaboresha mali asili ikiwamo misitu na ardhi.

Akasisitiza kwamba,  juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ni juhudi mtambuka zinazopashwa kumshirikisha na kumjumuisha kila mutual kuanzia mtu wa kawaida ambaye haswa ndiye muathirika mkuu.

Bi.Helen Clark anaongeza kuwa Tuzo hiyo inatolewa katika kipindi ambacho Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali wanakusanyika Jijini New York  kwa mkutano wao maalum wa kupitisha Ajenda 17   za Maendeleo Endelevu, ambapo ajenda namba 13 inazungumzia kwa kina mabadiliko ya tabia nchi wakati ajenda namba 15 inazungumzia uhifadhi wa viumbe hai, Misitu na kukabiliana na jangwa

Akasema Mkutano huu wa kupitisha ajenda za maendeleo endelevu zinazochukua nafasi ya malengo ya maendeleo ya millennia yanayomaliza muda wake mwaka huu, unatangulia mkutano mwingine muhimu unaosubiriwa kwa shauku kubwa ,  mkutano wa Mbadiliko ya Tabia nchi ( COP21).

MJUMITA ni kati ya  NGO Sita kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, zilizojinyakulia tuzo hiyo. NGO nyingine zilizoshinda Tuzo Nane zinatoka   Asia na  Pacific na   NGO nyingine Nane ni kutoka   Latin Amerika na Visiwa vya Karibbean

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.