
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Welezo Ndg Iddi Rwambo akizungumza na Wananchi na Wanachama wa CCM wakati wa Mkutano wa kuwatambulisha Wagombea wa CCM wa Jimbo hilo katika Mkutano wa Kampeni za Jimbo hilo katika viwanja vya Welezo Unguja.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ndg.Paul Makonda akiwahutubia Wananchi wa Jimbo jipya la Welezo wakati wa Mkutano wa Kuwatambulisha Wagombea wa CCM katika viwanja vya mpira Welezo Zanzibar.
Wagombea wa Nafasi za Ubunge na Uwakilishi Jimbo Jipya la Welezo Zanzibar wa kwanza Mhe Saada Mkuya, Waziri wa Fedha wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Ndg Hassan Khamis, wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, akihutubia mkutano huo wa utambulishi wa wagombea wa CCM katika viwanja vya mpira welezo Zanzibar.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ndg.Paul Makonda akiwatambulisha Wagombea wa Chama cha Mapinduzi wa Nafasi ya Ubunge Mhe Saada Mkuya na Uwakilishi Ndg. Hassan Khamis Hafidh, wakitambulishwa wakati wa mkutano wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya Welezo Zanzibar.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ndg.Paul Makonda akiwatambulisha Wagombea wa CCM wa Nafasi za Udiwani wa Jimbo la Welezo, Mgombea Udiwani wa Wadi ya Welezo Ndg Ramadhani Ali kulia na kushoto Mgombea wa Wadi ya Mtofaani Ndg Chum Shauri. wakitambulishwa kwa Wananchi katika Mkutano wa Kameni ya Wabunge katika viwanja vya Welezo Zanzibar.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mhe Saada Mkuya akiwasalimia Wananchi wakati wa kutambulishwa kwa Wananchi wa Jimbo la Welezo Zanzibar katika mkutano wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya Welezo.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Welezo Zanzibar wakiwaikiliza Wagombea wao wakati wa Mkutano wa Kampeni katika Jimbo hilo Jipya la Welezo Zanzibar.
No comments:
Post a Comment