Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk Shein, Auzindua Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar Michezani Zanzibar.

 Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar wazinduliwa rasmin na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein, kama unavyoonekana pichani wakati wa usiku ukipendeza na kupendezesha mandhari ya michezani Zenj.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na viongozi wa Serikali wakati akiwasili katika viwanja vya michezani kisonge kwa ajili ya uzinduzi wa Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee, wakiwa katika viwanja vya kisonge kwa ajili ua hafla ya uzinduzi wa Mnara huo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mshauri Elekezi wa Ujenzi wa Mnara huo Ndg Habib Nur akitowa maelezo ya ujenzi wa Mnara huo na majengo ya biashara yanayotaka kujengwa upande wa pili wa makontena michezani ikiwa ni mradi wa ZSSF.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Ndg Abdulwakil Haji Hafidhi , akitowa maelezo ya ujenzi wa majengo ya maduka katika eneo la michezani makontena ukiwa ni Mradi wa ZSSF katika uwekezaji wa miradi mbalimbali Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuuzindua Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa ufunguzi huo uliofanyika katika viwanja vya kisonge michezani Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kuuzindua Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimsikiliza mshauri wa maonesho ya chumba cha kumbukumbu cha maonesho ya katika Mnara huo Ndg Said El-Gheithy, ambaye ni mtaalamu wa mambo ya makumbusho Zanzibar. akitowa maelezo ya mti wa mkarafuu ulioko katika chumba hicho hauko pichani. 

Mtaalamu wa matayarisho ya moanesho katika ufunguzi wa Mnara wa Kumbukumbu Ndg Said El-Gheithy, akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, mchezo aliokuwa akiupenda Mzee Karume wa zuna, ni moja ya vitu vya kumbukumbu katika chumba cha maonesho ya kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipata maelezo ya baskeli ambayo ametumia Mzee Karuma katika kupigania mapinduzi ya Zanzibar ikiwa katika chumba cha maonesho ya kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar nac Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipata maelezo ya Kanga mbalimbali zilizotimika katika harakati ya Mapinduzi ya Zanzibar kupelea ujumbe kwa wananchi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Afisa Habari na Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Ndg Mussa Yussuf akiwa katika chumba maalum kwa ajili ya kuoneshea picha za kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Mama Mwanamwema Shein, na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif wakimsikiliza Mshauri Elekezi wa Ujenzi wa Mnara huo Ndg Habib Nur akitowa maelezo ya Mnara huo wakiwa sehemu ya juu ya Mnara ambayo itakuwa na mgahawa wa aina yake wa kuzunguka mnara huo 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipata maelezo ya Darubini maalumu ya kuvuta masafa marefu ikiwa juu ya mnara huo kutoka kwa Mshauri Elekezi wa Ujenzi kutoka Kampuni ya Habconsult Tanzania Ndg Habab Nur.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa juu ya Mnara huo, akiangalia maeneo ya mandhari ya Zanzibar kwa kutumia darubini maalum ilioyoko juu ya Mnara huo kwa ajili ya Wananchi na Wageni wanaotembelea Mnara huo wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif wakiwa katika viwanja vya michezani wakitoka kutembelea Mnara huo baada ya ufunguzi wake uliofanywa na Rais wa Zanzibar Dk Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasalimia Wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mnara wa Kumbukumbu ya Miako 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na kushoto Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.