Habari za Punde

Swala ya Pamoja na Dua Kuiombea Amani Zanzibar katika Uchuguzi Mkuu wa Zanzibar, Iliofanyika katika Viwanja vya Wete Pemba.


Kadhi wa Wilaya ya Wete Mohammed Ali Hamda, akiswalisha swala ya pamoja ya laasi iliyoambatana na dua ya kuombea nchi amani kuelekea katika uchaguzi mkuu, swala hiyo iliyofanyika katika viwanja vya jadida Wete Mkao wa kaskazini Pemba.
Waumini mbali mbali wa dini ya Kiislamu Wilaya ya Wete wakiwa katika swala ya pamoja huko katika viwanja vya Jadida Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, swala hiyo iliyoambatana na dua ya kuiombea nchi amani
Waumini mbali mbali wa Dini ya Kiislamu Wilaya ya Wete, wakisikiliza nasaha zilizokuwa zikitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Wete Mhe:Hassan Khatib Hassan hayupo pichani, mara baada ya kumalizika kwa dua ya kuombea nchi amani huko katika viwanja vya Jadida Wete Kisiwani Pemba
 Amiri wa Jumuiya ya JUMAZA Wilaya ya Wete Shekh Ghazal Abdalla, akitoa nasaha zake kwa wa Umini mbali mbali wa Dini ya Kiislamu, wakiofika kuitikia dua ya Pamoja ya kuiombea nchi amani kuelekea Uchaguzi Mkuu katika kiwanja cha Jadida Wete Pemba 

 Kadhi Mkuu wa Wilaya ya Wete Mohamed Ali Hamad, akizungumza na waumini wa dini Dini ya Kiislamu, wakiofika kuitikia dua ya Pamoja ya kuiombea nchi amani kuelekea Uchaguzi Mkuu katika kiwanja cha Jadida Wete Pemba
Kadhi Mkuu wa Wilaya ya Wete Mohamed Ali Hamad, akiomba dua ya mara baada ya kumalizika kwa swala ya Pamoja iliyoswaliwa katika Viwanja vya Jadida Wete Pemba, swala hiyo iliyoambatana na dua ya Pamoja ya kuiombea nchi amani kuelekea Uchaguzi Mkuu katika kiwanja cha Jadida Wete Pemba


Waumini mbali mbali wa dini ya Kiislamu wanawake wakiitikia dua ya kuombea nchi amani kuelekea Uchaguzi Mkuu, dua hiyo iliyotolewa na Shekh Massoud Shaaba ambaye hayupo pichani, huko katika viwanja vya Jadida Wete Pemba
Mkuu wa Wilaya ya Wete Mhe:Hassan Khatib Hassan katikati, akiungana na waumini mbali mbali wa dini ya Kiislamu katika kuitikia dua ya pamoja ya kuiombea nchi amani, dua hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Jadida Wete Kisiwani Pemba.
(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.