Habari za Punde

Benki ya Posta Tanzania Yakabidhi Kituo cha Afya Pemba

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa PIli wa Rais Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Wete Mhe: Hassan Khatib Hassan, mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Ungi Mkusa Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, akisalimia na viongozi mbali mbali wa Benk ya Posta Tanzania mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Ungi Msuka Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Bwana Sabasaba Moshingi wakati alipowasili katika kijiji cha Ungi Msuka Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, akiondoa kitambaa kuachiria uwekaji wa jiwe la msingi kituo cha Afya Ungi Msuka, Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Mkamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, akikata utepe pamoja na Mwenyekiti wa Bodi wa Benk ya Posta Tanzania Prifesa Lettice Rutashobya, kuashiria kukabidhiwa Serikali kituo hicho kwa hatua za mwisho zilizobakia.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Benk ya Posta Tanzania Bwana Sabasaba Moshingi, akitoa maelezo juu ya Chumba maalumu cha kutoa huduma za afya ya mama na Mtoto, kilichomo ndani ya kituo cha afya cha Afya Ungu Msuka Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.
Mwanakijiji wa Ungi Msuka Mwadini Habibu akisoma risala ya wanakijiji hicho, kabla ya kuwekewa jiwe la msingi kituo cha Afya kilichopo kijijini kwao huko Ungi Msuka Wilaya ya Micheweni kisiwani Pemba.
Mwakilishi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Jimbo la Konde Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba, Ismail Ali akitosa salamu za wanajumuiya wenzake wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kituo cha Afya kijijini kwao huko Ungi Msuka.

Afisa Mdhamini Wizara ya Afya Pemba Dk.Mkasha Hija Mkasha, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ungi Msuka Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.
Meneja wa Benki ya Post Tanzania tawi la Pemba, Issa Abdull akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ungu Msuka Wilaya ya Micheweni
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benk ya Posta Tanzania Bwana Sabasaba Moshingi, akisoma risala ya Benk hiyo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la kituo cha Afya Ungu Msuka Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benk ya Posta Tanzania Profesa Lettice Rutashobya, azungumza na wanakijiji wa Ungi Msuka kabla ya kuwekwa kwa Jiwe la msingi Kituo cha afya kijijini hapo

Mkuu wa Wilaya ya Wete Mhe:Hassan Khatib Hassan, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ungi Msuka Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba, kabla ya kuwekewa jiwe la msingi kituo chao cha afya kijiji hapo, kilichojengwa na Benk ya Posta Tanzania.
Waziriwa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, wapili kutoka kulia mwenye miwani akiangalia ratiba ya shuhuli ya uwekaji wa jiwe la Msingi kituo cha afya katika kijiji cha Ungi Msuka Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ungi Msuka Wilaya ya Micheweni Kiswani Pemba.
Watendaji wa Benki ya Posta Tanzania wakiwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya znaizbar, wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ungi Msuka Wilaya ya Micheweni kabla ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha afya kijijini hapo.

Wananchi wa kijiji cha Ungi Msuka Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba, wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, alipokuwa akizungumza na wananchi hao kabla ya kuweka jiwe la msingi kituo cha afya kijijini hapo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Banke ya Posta Tanzania, Mkuu wa Wilaya ya Wete Mhe:Hassan Khatib Hassan na akinamama wa Ungi Msuka mara baada ya kukabidhiwa Serikali kituo hicho.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.