Mkuu wa kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu B
iliyopo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, Fredrick
Nisajile akiongea na wakimbizi walio katika mpango wa kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta,
Mtendeli na Karago.Wakimbizi hao waliopokelewa kutoka nchini Burundi
hivi karibuni kwa sasa wanahifadhiwa kwa muda katika kambi ya Nyarugusu.
Wakimbizi kutoka nchini Burundi
wakipanga mizigo yao katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambayo wamehifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta,
Karago na Mtendeli ikiwa ni mkakati unaoratibiwa naWizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la
kushughulikia Wakimbizi (UNHCR)
na mashirika mengine ya kimataifa ili kuwapatia makazi salama.
Mtoto Jamine Nibetanga(14), kutoka nchini Burundi
akiandaa chakula katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B
iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambayo wakimbizi kutoka nchini Burundi
wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Karago na Mtendeli.
Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Kukimana Dafroza (katikati),
akifuma kikapu kama alivyokutwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B
iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wakimbizi kutoka Burundi
wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa katika kambi nyingine.
Wengine ni Mkabanura Eviline (kushoto) na Niragira Dafroza (kulia).
Watoto wa wakimbizi kutoka nchini Burundi
wakichota maji jana katika moja ya vituo vya maji vilivyowekwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu
B iliyoko wilayani Kasulu Mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa muda. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inampango wa kuwahamishiwa katika kambi za Karago,
Mtendeli na Nduta ili kupunguza msongamano uliopo katika Kambi ya Nyarugusu.
Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Jacqueline Elulu
(mwenyemtoto), akisubiri kupata huduma ya afya katika kituo cha Red Cross
kinachotoa huduma za afya kwa wakimbizi walioko katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Shirika la Red Cross
ni moja wapo ya wadau wanaoshirikiana na Serikali kutoa huduma za afya katika kambi ya Nyarugusu.
Mkimbizi
Joseph
Mtagura aliyeko katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu akiandaa mihogo ya kuwauzia wakimbizi wenzake wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma
Mkimbizi kutoka nchini Burundi,
Ntirampeba Acquelina akianika mihogo ambayo huwauzia wenzake katika kambi ya Nyarugusu B
iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Ugali wa mihogo ni mojawapo ya vyakula muhimu vinavyotumika katika kambi ya Nyarugusu.
Watoto wa wakimbizi kutoka nchini Burundi
wanaohifadhiwa katika kambi ya Nyarugusu wakicheza mpira kama walivyokutwa jana na mpigapicha wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wakimbizi hao wamekuwa kiingia nchini kutoka na machafuko ya kisiasa yaliyotokea nchini
Burundi hivi karibuni.
Wakimbizi kutoka Burundi
walioko katika Kambi ya Nyarugusu wakiandaa mboga ya kisamvu kama walivyokutwa na mpigapicha wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi aliyeko katika ziara ya kambi hiyo.
Mkimbizi Haverimana Ejide (kushoto) na Mkewe Kugimana Evona pamoja na watoto wao wakipata chakula cha
mchana katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B,iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa maeneo mengine ili kupunguza msongamano uliopo katika kambi ya Nyarugusu.
(PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA
NDANI YA NCHI)
No comments:
Post a Comment