Habari za Punde

Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, Jimbo la Paje Unguja Mkoa wa Kusini Unguja.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Abdalla Ramadhani akiwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya mpira Paje.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika viwanja vya mkutano Wilaya ya Kusini Unguja, uliofanyika katika viwanja vya Paje. 
Wanachama wa CCM wakishangiliwa wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar iliofanyika katika viwanja vya Paje Wilaya ya Kusini Unguja.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai akiwahutubia Wanachama wa Chama cha Mapinduzi katika viwanja vya Paje na kuwataka Wananchi kuipatia ushindi CCM ili kuendeleza Amani na Utulivu na maendeleo katika maendeleo ya Zanzibar.
Mzee Abdurazak Kwacha akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja na kuwataka kumchagua Dk Ali Mohamed Shein, kwa kura nyingi za Ndio ili kuendelea kuleta maendeleo kwa Wananchi wa Zanzibar.
Kada wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mgombea Uwakilishi Jimbo la Chwaka Mhe. Issa Haji Gavu akiwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viwanja vya mpira Paje Wilaya ya Kusini Unguja. 

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe Shamsi Nahodha Vuai akiwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, na kuwata Wananchi kuipa Ushindi CCM kupitia Mgombea Wake wa Urais Dk Ali Mohed Shein, ili kuendeleza kukamilisha Ilani ya CCM kwa maendeleo ya Wazanzibar katika kipindi cha Pili cha Uongozi wake.
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM Dk Sira Ubwa Mwaboya akiwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja na kuwataka kukipigia Kura za Ndio Chama cha Mapinduzi ili kuleta maendeleo katika Sekta mbalimbali za Jamii. Akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo wa mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viwanja vya mpira Paje Wilaya ya Kusini Unguja.  
Mwanachama wa CCM Ndg Peter Sipano akishangilia wakati wa mkutyano huo wa kampeni katika viwanja vya mpira Paje Unguja.akishangilia kwa staile yake. 
Mjumbe wa Kamati Kuu wa CCM Balozi Seif Ali Iddi, akiwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viwanja vya mpira Paje Wilaya ya Kusini Unguja. 
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja akiwa katika mikutano yake ya kampeni kuomba ridhaa za Wananchi kumchagua kwa kipindi cha pili kuiongoza Zanzibar kwa maendeleo na kuimarisha sekta za Uchumi wa Zanzibar katika sekta mbalimbali.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakimshangilia Mgombea Urais wa Zanzibar wakati akiwahutubia katika mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Paje Wilaya ya Kusini Unguja.
Wananchi wakimsikilizac Mgombea wa Urais wa Zanzibar wakati akitangaza Sera za Ilani ya CCM kwa kipindi cha Miaka mitano ya Uongozi wake wakati wa mkutano wake wa kampeni katika viwanja vya mpira Paje Wilaya ya Kusini Unguja na kuomba kura ili kuiongoza Zanzibar kwa maendeleo na kudumisha Amani na Umoja katika Zanzibar. 
Wagombea Ubunge na Uwakilishi wa Jimbo la Paje Wilaya ya Kusini Unguja wakimsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Paje Wilaya ya Kusini Unguja.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Paje kupitia CCM Ndg Jaffar Sanya wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya mpira Paje Wilaya ya Kusini Unguja.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi Jimbo la Makunduchi kupitia CCM Ndg. Haji Ameir Timbe,wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya mpira Paje Wilaya ya Kusini Unguja.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakishangilia wakati Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea wa Uwakilishi, Ubunge na Udiwani kupitia CCM, katika viwanja vya mpira Paje. Wilaya ya Kusini Unguja. 
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi Jimbo la Makunduchi, kupitia CCM Mhe. Haroun Ali Suleiman, wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya mpira Paje Wilaya ya Kusini Unguja.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi Jimbo la Paje kupitia CCM Mhe. Hashim Jaku, wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya mpira Paje Wilaya ya Kusini Unguja.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Wagombea Udiwani wa Wilaya ya Kusini Unguja,kupitia CCM.wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya mpira Paje Wilaya ya Kusini Unguja.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakishangilia wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya mpira Paje Unguja.
Msanii wa Kizazi Kipya Zenj Flava Baby J akitowa burudani wakati wa mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya mpira Paje Unguja.
Wasanii wa Bendi ya Yamoto wakilishambulia jukwaa wakati wa mkutano wa kampeni ya mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein. katika viwanja vya mpira Paje Wilaya ya Kusini Unguja.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakishangilia wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya mpira Paje Unguja.
Wanachama wa CCM wakisherehekea kushangilia wakati Bendi ya Yamoto ikitowa burudani katika viwanja vya mkutano wa kampeni ya mgombea Urais wa Zanzibar uliofanyika Mkoa wa Kusini Unguja.
Wasanii wa Bendi ya Moto wakitowa burudani wakati wa mkutano huo wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar katika viwanja vya mpira Paje Unguja.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakishangilia wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya mpira Paje Unguja.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiagana na Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kumaliza mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Paje Unguja.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiangana na Wananchi waliohudhuria mkutano wa Kampeni katika viwanja vya mpira Paje Unguja.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot. Zanzinews.com.
                                                    Email.othmanmaulid@gmail.com.
                                                    Mobil.0777424152. Or 0715424152.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.