Habari za Punde

UNESCO Yakutanisha Wadau Kujadili Amani Uchaguzi Mkuu.

UN 1
Katibu Mkuu wa Baraza la Mahedhebu kwaajili ya Amani,Mchungaji,Canon Thomas Godda akizungumza katika kongamano la Amani lililoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO)kwa kushirikiana na madhehebu ya Dini na Viongozi wa Mila ili kuhamasisha amani katika kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Na Mwandishi wetu, Simanjro
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia na Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) limekutanisha wadau mbalimbali katika kongamano la kujadili na kuhamasisha amani katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 4,2015
Kongamano hilo lilifanyika katika Kituo cha Redio Orkonerei (ORS)Terrat wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara na kuwaleta pamoja viongozi wa dini,mila na wawakili wa muungano wa Redio za Jamii nchini(Comneta)ambao kwa pamoja walisisitiza umuhimu wa amani.
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph alisema mchango wa unaotolewa na Redio za kijamii nchini ni mkubwa kwani unawawezesha wananchi kuzitumia kujiletea maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya kuhamasisha amani na utulivu katika kipindi hiki na baada ya uchaguzi mkuu.
Ameongeza kuwa Muungano wenye nguvu wa Redio za Jamii ndio ukombozi wa wananchi kwani wanahitaji kuelimishwa maswala mbalimbali ya afya, kilimo na programu zinazoandaliwa na serikali kwajili ya wananchi.
Mmoja wa viongozi wa mila ,Laigwanani Lesira Samburi alisema viongozi wa mila licha ya mchango wao kwenye jamii bado hawajashirikishwa ipasavyo pamoja kuwa huwa hawajishughulishi na siasa moja kwa moja.
"Naomba serikali itambue mchango wetu katika kutatua migogoro na kuhamasisha amani kwenye jamii zetu,tunaweza kufanya mambo makubwa kama serikali ikitushirikisha ipasavyo sio katika kipindi hiki cha uchaguzi tu bali hata baada ya uchaguzi,"alisema Samburi
UN 2
Mwenyekiti wa Radio za Jamii kutoka UNESCO na Mhadhiri Mwandamizi wa Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Hyderabad, Profesa Vinod Pavarala akizungumza katika kongamano la amani, lililofanyika katika Kituo cha Redio ya Jamii ya ORS (OPA)iliyopo wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara. Pichani wanaofatilia kwa karibu ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Dini kwa ajili ya Amani, Mchungaji Thomas Godda na Afisa Miradi wa UNESCO, Al-Amin Yusuph.

Nae Katibu Mtendaji wa Baraza la Dini kwaajili ya amani, Mchungaji Thomas Godda alisema viongozi wa mila wana michango muhimu kwani wako karibu sana na jamii inayowazunguka hivyo wakishirikiana na viongozi wa madhehebu ya dini na asasi za kiraia kuna mambo ya msingi yatakayoipa jamii heshima .
Alisema Tume ya uchaguzi imewashirikisha katika hatua muhimu wadau wake kuhakikisha kila mwananchi aliyejiandikisha anapata haki ya kupiga kura na hakuna udanganyifu utakaotokea hivyo kuwataka wananchi washiriki kwa amani tukio hilo muhimu katika kukuza demokrasia nchini.
Mjumbe wa bodi ya Muungano wa Redio za Jamii nchini (COMNETA), Balozi Christopher Liundi alisema iwapo wananchi watazitumia ipasavyo redio za jamii zitaleta mabadiliko chanya.
UN 3
Mjumbe wa Bodi ya Muungano wa Redio za Jamii nchini (COMNETA), Balozi Christopher Liundi akichangia mada ya umuhimu wa matumizi ya Redio za Jamii.
UN 4
Kiongozi wa Mila ya jamii ya wafugaji katika Kijiji cha Terrat wilaya Simanjiro mkoa wa Manyara, Lesira Samburi akizungumza kwenye kongamano la kuhamasisha amani kuelekea Uchaguzi Mkuu.
UN 5
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Redio ya Jamii 94.9 Mkoani,Pemba,Hamdu Hasan Bakari (kushoto)akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Dini kwa ajili ya Amani, Mchungaji Thomas Godda.
UN 11
Meneja wa Orkonerei Radio Service Simanjiro Manyara (ORS FM), Bw. Baraka Ole Maika akivishwa Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph mavazi ya jamii ya wafugaji wa kimaasai ikiwa ni ishara ya kumpongeza na kumuaga baada kuhamishwa kikazi nchini India, kushoto ni Mwenyekiti wa Muungano wa Redio za Jamii nchini (COMNETA), Joseph Sekiku.
3 (2)
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph (kulia) akifurahia zawadi ya mavazi na Rungu la jamii ya wafugaji wa kimaasai na kusimikwa rasmi kuwa 'Laigwanan' kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza jamii hiyo kupitia Redio za jamii nchini, Al Amin amepewa uhamisho kwenda India, kushoto ni Kiongozi wa Mila, Laigwanan Lesira Samburi na Mwenyekiti wa Muungano wa Redio za Jamii (COMNETA) Sekiku Joseph.
amani
Viongozi wa Mila wakionesha ujumbe wa kuhamasisha amani.
UN 6
Katibu Mtendaji wa Baraza la Dini kwaajili ya Amani, Mchungaji Thomas Godda (kushoto) akiteta jambo na maafisa wa UNESCO, Nancy Kaizirege na Al -Amin Yusuph.
UN 8
Ujumbe wa Muungano wa Redio za Jamii,Wazee wa Mila na Viongozi wa dini wakiwasili kwenye kiwanda cha kuzalisha nishati kwa njia ya Mibono katika Kijiji cha Terrat ambacho kimekua msaada kwa wananchi wengi.
UN 7
2 (1)
Mkurugenzi wa Kituo cha Redio ya Jamii ya ORS (OPA)iliyopo wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara,Martin Kariongi (kushoto) akizungumza na ujumbe ulioshiriki kongamano la amani lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshighulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) waliotembelea mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia teknolojia ya Mafuta ya Mibono.
UN 9
Mbegu zinazotumika kuzalisha mafuta kwa ajili ya nishati.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.