Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar Xie Yunliang akitoa maelezo wakati wa sherehe ya kukabidhi msaada wa dawa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500 zilizotolewa na Jimbo la Jiangsu kwa ajili ya Wananchi wa Zanzibar. Sherehe hiyo ilifanyika Bohari Kuu ya Madawa Maruhubi Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Madaktari wa China na waalikwa wakifuatilia sherehe ya makabidhiano ya msaada wa dawa mbali mbali za binaadamu katika sherehe iliyofanyika Bohari Kuu ya Madawa Maruhubi.
Kamishna wa Afya na Uzazi wa Mpango ambae pia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Jimbo la Jiangsu Hong Hao akizungumza wakati wa makabidhiano ya dawa zenye thamani ya shilingi milioni 500 (kulia) Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabiti Kombo.
Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar Xie Yunliang na Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo wakitia saini makabidhiano ya dawa hizo zilizotolewa na Jimbo la Jiangsu.
Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na Balozi mdogo wa China wakibadilishana hati za makabidhiano ya msaada wa dawa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500 katika sherehe zilizofanyika Bohari Kuu ya Madawa Maruhubi.
No comments:
Post a Comment