Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Ali Khamis Juma kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha kabla aklikuwa Naibu katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji Uataswi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar,hafla ya kiapo hicho ilifanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba Nd,Abeid Juma Alina Naibu Katibu Mkuu Wizara ya FedhaNd,Ali Khamis Juma leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu mpya wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini PembaNd,Abeid Juma Ali (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nd,Ali Khamis Juma (kulia)baada ya kuwaapisha kushika nyadhifa hizo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.{Picha na Ikulu}
STATE HOUSE
ZANZIBAR
OFFICE OF THE
PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 7.12.2015

RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha Ndugu Abeid Juma Ali, kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Micheweni Pemba.
Wakati huo huo, Dk. Shein amemuapisha ndugu Ali Khamis Juma, kuwa Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar
na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria katika hafla hiyo ni Dk. Mwinyihaji
Makame Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala Bora, Waziri wa Fedha
Mhe. Omar Yussuf Mzee, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara
Maalum Mhe. Haji Omar Kheir, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassn Said .
Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis
Haji, Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Meya wa Manispaa ya Mji
wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib,Washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi
wengine wa Serikali.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment