Sehemu ya kuingilia ndani ya Studio hiyo ya Hit Fm ikiwa imeteketea kwa moto
Vifaa vya kutangazia katika Studio hiyo vikiwa vyote vimeteketea kwa moto huo, uliosababishwa na Watu wasio julikana usiku wa juzi.na kuteketea kwa vifaa vyote vya utangazaji katika Studio hiyo ilioko Migombani Mjini Zanzibar. baada ya kuvyamiwa na watu wasio julikana na kutenda hujuma hiyo.
Waandishi wa habari wakitembelea Studio hiyo kuagalia uharibifu ulitoyokea
Mmiliki wa Redio Hit Fm Mohammed Abdalla akiongozana na Viongozi waliotembelea Studio yao na kujionea uharibifu uliotokea kwa moto huo.
Waandishi na Wananchi waliofika kujionea moto uliounguza kituo hicho cha Redio cha Hit Fm kilichoko migombani Zanzibar.
Mwandishi akimuhoji Mkuu wa Utawala wa Afisi Kuu ya CCM alipofika kuangalia kituo hicho cha Hit Fm kujionea hasara iliopata kituo hicho
Mmiliki wa Kituo hicho cha Hit Fm Mohammed Abdalla Mohammed akizungumza na waandishi wa habari kutokana na hasara aliyoipata kwa moto huo na kulaani kitendo hicho cha kutiliwa moto studio yake na kuweza kupata hasara kutokana na kuunguwa kwa vifaa vya studio hiyo.
Meneja wa Redio ya Hit Fm Hafidh Kassim akizungumza na waandishi wa habari hasara walipata kutokana na moto huo na kukosa kuwa hewani kwa matangazo yake kama kawaida. Na kulaani kitendo hicho cha kuchomewa Studio yao kimefanya kuwakosesha ajira Wafanyakazi wa Kituo hicho.
Mkuu wa Atawala wa Kampuni ya Zanzibar Cable akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali viliko Zanzibar kuhusiana na janga hilo la kuchomwa kwa Kituo cha cha Redio cha Hit Fm na kusababisha hasara ya shilingi karibu milioni 65 kwa kuugua kwa vifaa vya utangazaji katika studio hiyo, wakayi ikiwa hewa na kuvamiwa na Watu wasiojulikana, katika ajali hiyo wafanyakazi wamepata majaraha.
Waandishi wakifuatilia kwa makini maelezo yanayotolewa na Mkuu wa Utawala Kampuni hiyo inayomiliki Kituo hichi Zanzibar Cable akitowa maelezo ya hasara iliopatikana kutokana na kuungua kwa Studio hiyo.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakifuatilia taarifa hiyo ya ajali ya moto ya Kituo cha Redio cha Hit Fm kutiwa moto na Watu wasiojulikana.
Meneja wa Baraza la Habari Tanzania MCT Zanzibar Suleiman Seif akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusiana na kutiwa moto kituo cha Redio cha Hit Fm Zanzibar na Watu wasiojulikana usiku wa manani juzi 2 disemba.2015, kushoto mtangazaji wa kituo hicho.
Hao watu bilashaka wanajulikana na wametumwa wafanye hicho kitendo kwa maslahi ya kisiasa tu hakuna jengine, kijinchi kidogo wakazi wake hawazidi milioni 2 lakini balaa zake hazitokei popote ulimwenguni kwa sababu ya wanasiasa waovu.
ReplyDelete