Afisa Mdhamini Elimu Pemba, Salum Kitwana Sururu akifungua mafunzo ya utayarishaji wa Katiba na
sheria kwa wanafunzi wa skuli za sekondari Pemba, amabao ni wanachama wa vilabu
kadhaa kisiwani humo, kulia ni Mratibu wa mafunzo hayo Mohamed Hassan Ali na
kushoto ni Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar tawi la Pemba, Fatma
Khamis Hemed
Fatma Khamis Hemed wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, akiwaonyesha katiba ya
Zanzibar ya mwaka 1984, wanafunzi wa skuli za sekondari Pemba, ambao ni
wanachama wa vilabu mbali mbali, ikiwa ni pamoja na mazingira na sayansi, kwenye
mafunzo ya utayarishaji wa katiba na sheria
Mratibu wa
mafunzo ya utayarishaji wa katiba na sheria Mohamed Hassan Ali, akiwa makini
kusikiliza michango ya wananfunzi ambao ni wanachama wa vilabu kadhaa,
akifuatiwa na Aisa Mdhamini elimu, Salum Kitwana Sururu.
Wanafunzi wa vilabu kadhaa ikiwa ni pamoja na sayansi wa skuli za sekondari Pemba, wakisikiliza mada zilizowasilishwa kwenye mafunzo yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC kisiwani Pemba, juu ua utayarishaji wa katiba na sheria
Mtoa mada
Mohamed Hassan Ali, akiwasilisha mada juu ya haki za binadamu, kwa wanafunzi wa
skuli za sekondari ambao ni wanachama wa vilabu kadhaa, mafunzo hayo
yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, na
yalifanyika afisini kwao mjini Chakechake
Khalfan Amour
Mohamed wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, akiwasilisha mada ya
udhalilishaji, kwa wanafunzi wa skuli za sekondari Pemba, ambao ni wanachama wa
vilabu mbali mbali ikiwa ni pamoja na mazingira na sayansi, kwenye mafunzo ya
utayarishaji wa katiba na sheria
Mwanafunzi anaesoma darasa la kumi (FII), skuli ya
Connecting Chakechake, akielezea namna ambayo mafunzo ya utayarishaji wa katiba
na sheria, jinsi atakavyo yafikisha kwa wanafunzi wenzake na jamii kwa ujumla, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
No comments:
Post a Comment