Habari za Punde

Bunge la Nne la Vijana Zanzibar.

SPIKA wa Bunge la Vijana akiingia katika Ukumbi wa Bunge la Vijana kuaza Kikao hicho cha Bajeti kwa mwaka wa Fedha kujadili bajeti za Wizara mbalimbali, Bunge hilo limefanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa zamani kikwajuni Zanzibar.
MAWAZIRI wa Wizara mbalimbali wakiwa wamesimama wakati Spika wa Bunge la Vijana akiingia ukumbini kuaza kwa Kikao cha Bunge katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa zamani kikwajuni Zanzibar.
SPIKA wa Bunge la Vijana Zanzibar Mhe. Mohammed Kassim, akisoma dau kabla ya kuaza kwa Kikao hicho cha Bunge la Vijana kilichofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni Zanzibar.

Wabunge wakiwa wamesimama wakati wa kusomwa kwa dua ya kabla ya kuaza kwa Kikao cha Bunge la Vijana Zanzibar.


WAZIRI wa Ajira Mhe.Machano Ali Machano akiwasilika bajeti ya Wizara yake kwa Wajumbe wa Bunge la Vijana wakati wa Kikao chake kilichofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa zamani Kikwajuni Zanzibar.

Mhe Waziri akitowa ufafanuzi wa jambo wakati wa Bunge hilo la Vijana Zanzibar. 
Mheshimiwa Mbunge akichangia wakati wa Bunge hilo la Vijana.

Waziri wa Fedha wa Bunge la Vijana Mhe. Salha Hamad akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake wakati wa Bunge la Vijana lililofanyika Ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar
Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Vijana wakibadilishana mawazo wakati wa Kikao hicho wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Bunge.
 Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Vijana wakifuatilia michango na hutuba ja bajeti zikiwasilishwa na Mawaziri husika.
Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Vijana wakiwa makini kufuatilia michani na Bajeti wakiti zikiwasilishwa katika mkutano huo wac Bunge la Vijana la nne  


Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Dk Yahya Khamis Hamad na Mwakilishi wa UNDP wakifuatilia Bunge hilo la Vijana Zanzibar, ambalo limeandaliwa na Afisi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la UNDP. 
WAZIRI wa Uchumi Mipango na Maendeleo Maalim Mohammed Said, akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake katika Kikao cha Bunge la Vijana Zanzibar kilichofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar.    
Waziri wa Uwekezaji Mhe Ali Haji Haji akisoma  bajeti ya Wizara yake wakati wa Bunge la Vijana Zanzibar. 

Mhe. Mbunge wa Bunge la Vijana akichangia wakati wa Kikao hicho cha Bunge. 
Spika wa Bunge la Vijana Zanzibar akitoka katika Ukumbi wa Bunge la Vijana baada ya kumalizika kwa mkutano wa nne wa Bunge la Vijana uliofanyika katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni, Bunge hilo limedhaminiwa na Afisi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa kushirikiana na UNDP 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.