Habari za Punde

Mashindano ya Resi za Ngalawa Wilaya ya Kati Unguja

Jumla ya ngarawa 18 zilishiriki katika mashindano ya asili ya resi za ngarawa yaliyofanyika jana kwenye kijiji cha Tindini, Unguja Ukuu jimbo la Tunguu Zanzibar.Katika mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka,Wenyeji Tindini waliingiza ngarawa 14 ambapo  Fumba, Dimani, Bungi na Kikungwi walileta ngarawa mojamoja.
Resi hizo za ngarawa zilivutia mamia ya wananchi ambapo mgeni rasmi, alikuwa mgombea Uwakilishi Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe.Simai Mohamed Said kwa niaba ya Mbunge wa jimbo hilo la Tunguu, alikabidhi zawadi kwa washindi watatu wa mwanzo.
 Mgeni rasmi Simai Mohamed Said akiongea na manahodha na wananchi waliohudhuria mashindano hayo
 Ngarawa zikianza mashindano hayo ya resi za ngalawa zilizofanyika katika pwani ya Unguja Ukuu Zanzibar zikiaza mashindano hayo hufanyika kila mwaka na kwa mwaka huu kushirikisha ngalawa 18..
Mgeni rasmin wa mashindano hayo ya ngalawa Mhe Simai Mohammed Said  akikabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mashindano hayo Nahodha Seif Dogo Mbungi.
 Simai Mohamed Said akifurahia jambo na watoto waliofika kuangalia resi za ngarawa jana.(Picha na Martin Kabemba)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.