Habari za Punde

Ujumbe kutoka Manispaliti ya Sundsvalls, Sweden Wawasili Zanzibar kwa Ziara ya Kawaida na Wenyeji Wao Makunduchi.

Mwalimu Hafith Ameir, Senior Citizen of Makunduchi akibadilishana mawazo na Bi Christin Stromberg, Mratibu, mara tu baada ya ujumbe wa Manispaliti ya Sundsvalls, Sweden kuwasili kwa ziara ya kikazi huko Makunduchi.

Kamati ya Wadi za Makunduchi imepokea wajumbe 4 wa vyama mbali mbali kutoka Manispaliti ya Sundsvalls, Sweden kwa ziara ya siku sita nchini. Ujumbe huo unaongozwa na Bwana Joao Pinheiro wa nne kutoka kushoto na upo nchini kwa ajili ya kuanza mashirikiano na Wadi za Makunduchi ambayo yatalenga zaidi upande wa elimu. Wengine kutoka kushoto ni Bi Christin Stromberg ambaye ni mratibu; Hans Zetterqvist, mwalimu Hafith Ameir ambaye ni Senior Citizen of Makunduchi; Anne-li Sjolund. Wengine waliofika kuwapokea wageni hao ambao hawapo kwenye picha ni ndugu Mohamed Muombwa; mratibu, mwalimu Haji Kiongo na ndugu Ali Khatibu.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.