Habari za Punde

Wazazi Kisarawe wafunguka kuhusu adhabu kwa watoto

 Joseph Olowa akiiomba kampuni ya True Vision kusaidia 
kuelimisha watu wenye lugha za matusi hadharani  hivi 
karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa 
watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production 
kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani 
kisarawe Mkoani Pwani.







  Mtoto akionesha jeraha alilopata baada ya kuchapwa na baba yake alipokuwa mdogo hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani.


Mkazi wa kisarawe  Juma Athumani akitoa ushuhuda wa adhabu ya kufukuza watoto nyumbani  hivi karibuni wakati 

wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto 

ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa 

ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto.


Cornel Anatory akielezea alivyomwagiwa maji ya ugali utotoni   hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani

Hamisi Idd akihamamisha wazazi kuwapa watoto elimu ya dini tangu utotoni ili kuepuka tabia mbaya hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani


Jamila Shabani akisema kuwa moja ya adhabu wanayopewa watoto ni kuchapwa fimbo    hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani

Kimela Billa Mtayarishaji wa vipindi vya Walinde Watoto akikabidhi Redio kwa Bi. Mwashamba Mrisho ambae ni mtendaji kata wa kata ya Kibo   hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani





Kikundi cha Kisarawe Bomani maarufu kama Kibo katika picha ya pamoja baada ya kupata redio kutoka True Vision hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani




Kikundi cha Tushirikiane cha Kisarawe wakijadiliana baada ya kupewa Redio na True Vision ili kufuatilia vipindi vya Walinde Watoto hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani

Na Krantz Mwantepele , Kisarawe 


Watanzania wametakiwa kuwa karibu na watoto wao na kujenga urafiki nao ili kuwawekea misingi bora ya nidhamu na upendo. Rai hiyo imetolewa na baadhi ya wazazi na walezi kutoka wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto.

Katika mdahalo huo mada mbalimbali zilijadiliwa zikiwemo athari za kuchapa watoto, matusi pamoja na adhabu kali kwa watoto mfano kuwafukuza watoto nyumbani.

Aidha washiriki wa mdahalo huo walionyesha kusikitishwa na vitendo vya kuchapa watoto fimbo kupita kiasi na wengine wakikemea tabia ya baadhi ya wazazi na walezi kutukana watoto pasipo kuzingatia maadili huku wakiiomba serikali kuwawajibisha wale wote wanaotukana hadharani bila kujali uwepo wa watoto.

Katika hatua nyingine, washiriki hao walikemea tabia ya kuwafukuza watoto nyumbani na kudai kuwa huo ni mwanzo wa kuwaingiza watoto katika matatizo makubwa na kuongeza idadi ya watoto wa mitaani aidha wamependekeza kuwa ni vyema watoto wafanyiwe maombi mara kwa mara na kuwashirikisha katika Ibada ili kuwaepusha kuwa na utovu wa nidhamu.

Kwa upande wao wanafunzi wa shule ya msingi Kibasila Kisarawe ambao walipata nafasi ya kuongea na timu ya Walinde Watoto walionyesha kuchukizwa na tabia ya kupewa adhabu kupita kiasi pamoja na kutukanwa tabia ambayo hufanywa na baadhi ya walimu na wazazi.


Naye mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kibasila Kisarawe Debora Mbalilaki alipendekeza kuangalia uwezekano wa kuwepo na adhabu mbadala badala ya fimbo kwa wanafunzi.




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.