Habari za Punde

ADC yakutana na Wagombea, mawakala na wanachama Pemba

 MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ADC Mhe: Hamad Rashid Mohamed, akiambatana na Kamishina wa chama hicho kanda ya Pemba Said Seif Said, wakiigia kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Amali Vitongoji Chakechek, tayari kuzungumza na wagombea, mawakala na wanachama wa chama hicho kuelekea uchaguzi wa marudio, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ADC Mhe: Hamad Rashid Mohamed, akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa chama hicho, wakipiga kofi, wakati walipoingia kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Amali Vitongoji Chakechake, kabla ya kuzungumza na wagombea, mawakala na wanachama wao, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 BAADHI ya wanachama wa ADC wakifuatilia mkutano uliohutubiwa na mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho Mhe: Hamad Rashid Mohamed uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Amali Vitongoji Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 MSOMA utenzi Shaniya Khamis katika mkutano uliohutubiwa na mgombea urais wa chama cha ADC Zanzibar Mhe: Hamad Rashid Mohamed, uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Amali Vitongoji Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

KAMISHANA wa chama cha ADC kanda ya Pemba Said Seif Said akieleza jambo kwenye mkutano wa chama hicho, uliohutubiwa na mgombea urais wao Mhe: Hamad Rashid Mohamed, uliofanyika Chuo cha Amali Vitongojia Chake chake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MLEZI wa chama cha ADC Pemba, Shoka Khamis, akizungumza kwenye mkutano wa wanachama, wagombea na mawakala wa chama hicho, uliofanyika Chuo cha Amali Vitongoji Chakechake Pemba, na kuhutubiwa na mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho Mhe: Hamad Rashid Mohamed, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ADC Hamad Rashid Mohamed, akizungumza na wanachama, wagombea na mawakala wa chama hicho, kwenye kutano wa hadhara, uliofanyika chuo cha Amali Vitongoji Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

1 comment:

  1. huyu si hana chama sasa atagombea bila ya chama?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.