Habari za Punde

Dk Shein amuapisha Makamu wa Pili wa Rais Ikulu

STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
RESS RELEASE
    Zanzibar                                                   30 Machi, 2016
---

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo  amemuapisha  Balozi Seif Ali Iddi kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Dk. Shein alimteua Balozi Seif Ali Iddi kushika wadhifa huo hivi karibuni kwa mujibu wa kifungu cha 39(2) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984.

Uteuzi wa Balozi Seif Ali Iddi ni uteuzi wa pili wa Mheshimiwa Rais tangu alipoapishwa Alhamisi iliyopita kuanza kipindi chake cha pili cha uongozi wa Awamu ya Saba.

Sherehe za kumuapisha Makamu wa Pili wa Rais ambazo zilifanyika Ikulu Zanzibar zilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na  Spika wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mheshimiwa Omar Othman Makungu na Mwanasheria Mkuu Mheshimiwa Said Hassan Said.

Wengine ni pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mufti Mkuu Sheikh Omar Kabi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Maghribi Abdalla Mwinyi Khamis na Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib.

Balozi Seif Ali Iddi anashika wadhifa huo kwa mara ya pili. Mara ya kwanza aliteuliwa mwezi Novemba, 2010 na kuushikilia hadi kumalizika kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya uongozi wa Awamu ya Saba kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 20 Machi, 2016.
  
Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.