Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati),
akisalimiana na wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa yanayohudumia
wakimbizi katika Kambi ya muda ya NMC, iliyoko mkoani Kigoma, kushoto ni
Mratibu wa Wakimbizi Mkoani Kigoma, Tonny Samwel
Laiser.Naibu Waziri yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
Mkuu
wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani Ofisi ndogo ya Kibondo,Dost Yousafzai
(kushoto), akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni(kulia), wakati ya ziara ya Naibu Waziri kutembelea
ilipokuwepo kambi ya wakimbizi ya Karago, wilayani Kibondo. Naibu Waziri yuko
mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wakimbizi wa Burundi (hawapo
pichani) wanaoishi katika kambi ya Mtendeli, iliyoko wilayani Kakonko mkoani
Kigoma.Naibu Waziri yuko Mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.(Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
No comments:
Post a Comment