Habari za Punde

Fainali ya Kombe la Ndondo Cup Theo Combain Waibuka Mabingwa wa Kombe hilo kwa Ushindi bao 2-1. Lililodhaminiwa na Kituo cha Redio cha Coconut fm Zanzibar. Kati ya Six Center na Theo Combain

Mkurugenzi Mkuu wa Coconut Fm Zanzibar Ali Dai akifuatilia mchezo huo wa Fainali ya Kombe la Ndondo Cup zilizoandaliwa na Kampuni ya Redio ya Coconut Fm Zanzibar na kushirikisha timu 18 katika mashindano hayo yaliofikia kilele katika mchezo wa Fainal kati ya Six Center na Theo Combine mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Wananchi na Wapenzi wa Mchezo wa Soka Zanzibar wakifuatilia Fainali ya Kombe la Ndondo Cup kati ya Six Center na Theo Combain mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Theo Combain imeshinda 2--1
Wapenzi wa mchezo wa Soka Zanzibar wakiwa wamefurika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar kufuatilia Fainal ya Kombe la Ndondo Cup iliozikutanisha Timu za Six Center na Theo Combain, Michuano hiyo ilikuwa Chini ya Udhamini wa Kampuni ya Redio ya Coconut Fm Zanzibar.
Benchi la Ufundi la Timu ya Theo Combain wakifuatilia mchezo huo
Benchi la Ufundi la Timu ya Six Center wakifuatilia mchezo huo
Mchezaji wa Timu ya Theo Combain akimpita mchezaji wa Timu ya Six Center.
Mchezaji wa Timu ya Theo Combain akimpita beki wa Timu ya Six Center wakati wa mchezo wao wa Fainali ya Kombe la Ndondo Cup mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Theo Combain imeshinda mchezo huo 2--1

Msanii Baby Jay akishuka jukwaani wakati wa mchezo wa Kombe la Ndondo Cup kutowa burudani kwa Mashabiki wa Mchezo wa Soka Kombe la Ndondo Cup zilifanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Msanii wa Zenj Flava Baby Jay akitowa burudani kwa Wapenzi wa Mchezo wa Soka Zanzibar waliohudhuria Fainali ya Kombe la Ndondo Cup kati ya Six Center na Theo Combain. Timu ya Theo Combaini imeshinda 2--1 
Mashabiki wa Muziki na Soka Zanzibar wakimshangilia Msanii wa Kizazi Kipya Baby Jay akitowa burudani wakati wa Fainal ya Kombe la Ndondo Cup. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.