Habari za Punde

JKU, Villa Kuhukumiwa na Wajibuti

Shirikisho la kabumbu barani Afrika(CAF) 


limewateuwa waamuzi wenye beji za FIFA kutoka 


nchini Djibouti kuchezesha pambano la awali kati ya 


Sports Club Villa Jogoo ya Uganda dhidi JKU ya 


Zanzibar.


Kupitia Shirikisho lao la mpira nchini Uganda (FUFA) 

Sports Club Villa tayari wamethibitisha kuwa 

pambano hilo litachezwa kwenye dimba la kimataifa 

la Mandela Jumamosi ya March 12 saa kumi alasiri.

Waamuzi hao ni Souleiman Ahmed Djamal, Abdillahi 

Mahamoud Iltireh, Hamze Abdi Salime, Djamal Aden 

Abdi na Kamisaa wa mchezo huo atakua Aweis 

Ahmed Jumal kutoka nchini Somalia.

Sports Club Villa imetinga hatua hiyo baada ya 

kuitoa Al Khartoum ya Sudan kwa ushindi wa jumla 

ya 2-0 kufuatia michezo miwili waliocheza.


Kwa upande wao JKU walifanikiwa kuingia nafasi 

hiyo bila ya jasho kutokana na wapinzani wao 

Gaborone United kutoka Botswana kujiengua kwenye 

kombe hilo la Shirikisho barani Afrika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.