Habari za Punde

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Apiga Kura Kituo cha Kiembesamaki Zanzibar

Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe Mahmoud Thabit Kombo alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Sekondari ya Kiembesamaki Zanzibar kwa ajili ya Kupiga Kura yake leo wakati wa Uchaguzi wa Marudio uliofanyika leo Mjini Zanzibar kumchagua Rais wa Zanzibar Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani. 
Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Fedha wa Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee, alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Sekondari ya Kiembesamaki Zanzibar kwa ajili ya Kupiga Kura yake leo wakati wa Uchaguzi wa Marudio uliofanyika leo Mjini Zanzibar kumchagua Rais wa Zanzibar Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani. 
Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akisubiri kukabidhiwa karatasi ya Kura kutoka kwa Karani wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Kituo cha Kiembesamaki Zanzibar.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akipiga Kura yake katika Kituo cha Kupigia Kura cha Skuli ya Sekongari ya Kiembesamaki Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar na Nje ya Zanzibar baada ya kupiga Kura yake katika Kituo cha Skuli ya Sekongari Kiembesamaki Zanzibar.
Mhe Samia Suluhu akiawapungia mikono wananchi waliofika katika uchaguzi wa Mardui wa Zanzibar uliofanyika leo baada ya kupiga kura katika Kituo hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mhe Jamuhuri Makamba akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar baada ya kumshindikiza Mhe Samia Suluhu. 
Mwananchi wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar akipiga Kura yake katika Kituo hicho.
Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki wakiangalia Majina yao katika Ubao wa majina ya Wapiga Kura wa Kituo hicho cha Skuli ya Msingi Kiembesamaki Zanzibar.
Mwananchi wa Jimbo la Kiembesamaki akipiga kura yake kituoni hapo leo asubuhi.
Mhe Waziri wa Fedha Zanzibar Omar Yussuf Mzee akiwa amembeba mmoja wa mpiga kura wa Jimbo la Kiembesamaki ambaye ni mgonjwa akimpandika katika gari baada ya kupiga kura yake.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.