Waandishi Habari kisiwani Pemba, wakimsikiliza
kwa makini Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Mahmoud Mussa Wadi, wakati
alipokuwa akifungua kongamano la amani katika nchi, kabla, wakati na baada ya
Uchaguzi, huko katika ukumbi wa skuli ya Madungu Sekondari.
Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Fadhil
Suleiman Suraga, akitoa mada ya nafasi ya waandishi wa habari kuelekea Uchaguzi
Mkuu, katika kongamano la siku moja la kuhimiza amani, kabla, wakati na baada
ya uchaguzi huko katika skuli ya Madungu Sekondari Chake Chake.
Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Mahmoud Mussa
Wadi, akifungua kongamano la siku moja juu ya kuihimiza
amani ya nchi, kwa waandishi
wa habari kisiwani Pemba,
huko katika skuli ya Mdungu Sekondari.
(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
No comments:
Post a Comment