Habari za Punde

Uchaguzi wa Marudio ni Suluhisho la Kutatua Mvutano wa Siasa Zanzibar- UVCCM

Umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) umesema uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika  Jumapili ya Machi 20 mwaka huu ndiyo sululisho la kutatua mvutano wa kisiasa uliopo nchini.
Umesema mvutano huo uliotokea baada ya Tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC kufuta matokeo utatatuliwa kwa njia ya kidemokrasia baada ya kufanyika uchaguzi huru na wa haki utakaofanikisha kupatikana viongozi watakaoweza kuongoza dola kwa miaka mitano ijayo.
Akizunguza na waandishi wa habari Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka amesema  malumbano, vurugu na vitisho kwa sasa havina nafasi bali wanasiasa waungane na kuwa wamoja kwa kuwahamasisha wananchi wenye sifa kutekeleza haki yao ya kidemokrasia na waliokuwa hawashiriki wasiwazuie watu wengine wanaotaka kupiga kura .
Amewataka wananchi kuchambua kwa kina hoja na mijadala inayojengwa na wanasiasa juu ya hatima ya maendeleo ya Zanzibar kisha wafanye maamuzi ya kuchagua viongozi wanaohisi wanafaa kuongoza dola.
Amesema kwa sasa kuna baadhi ya makundi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kusambaza uongo kuwa hali ya Zanzibar sio shwari wakati si sahihi.
Amesema ni vyema suala hilo kukemewa na wanaharakati kabla hazijaleta athari kwa nchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.