Habari za Punde

Balozi Seif azindua mtandao mpya wa teknolojia ya kisasa wa 4G wa Zantel

 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel Tanzania Bwana Benoit Janin akimpokea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kuzindua Mtandao mpya wa Teknolojia ya kisasa wa 4G hapo katika viwanja vya Mnara wa Kumbu kumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar Michenzani Mjini Zanzibar.

Nyuma ya Balozi Seif ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Balozi Ali Abeid Aman Karume na Nyuma ya Bwana Benoit ni Waziri wa Afya Mh. Mahmoud Thabit Kombo.
 Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Balozi Ali Karume na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakifurahia jambo kwenye uzinduzi wa mtandao Zantel wa 4G.

 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel Tanzania Bwana Benoit Janin akiteta na Waziri wa Afya Mh. Mahmoud Thabit Kombo kwenye hafla hiyo fupi.
 Warembo wa Kampuni ya Zantel wakifuatilia tukio la uzinduzi wa mtandao wa 4G kwenye simu zao za mikononi zitakazowawezesha kupata huduma mbali mbali ikiwemo kuonanan na yule watakayempigia.

 Balozi Seif akipokea zawadi maalum kutoka kwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel Tanzania Bwana Benoit Janin mara baada ya kuzindua mtandao wa 4G wa Kampuni hiyo.

Nyuma ya Balozi Seif ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Balozi Ali Abeid Amaan Karume.
Balozi Seif Wa Tatu kutoka Kushoto akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Zantel, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi na wageni wengine walioalikwa kwenye uzinduzi wa Mtandao wa 4G.

Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Ujenzi Balozi Ali Karume na Katibu Mkuu wake Dr. Juma Malik na kushoto ya Balozi ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya   Zantel Tanzania Bwana Benoit Janin, Waziri wa Afya Mh. Mahmoud Thabit Kombo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipando Nd. Khamis Mussa Pamoja na Afisa muandamizi wa Kampuni ya Zantel hapa Zanzibar Ndugu Baucha.

Picha na – OMPR – ZNZ.

1 comment:

  1. Hivi hii serikali ina será gani za mawasiliano ? Hio Zanztel si wameuziwa Tigo kwa dola 1 ( moja)? Je ndo wameshindwa kuinunua wao SMZ kwa hio dola 1 ? maana wateja inao na miundombinu ipo, hata kama wangesema SMZ haitaki kuendesha kampuni ya simu, basi ule waya wa fibre na lile dishi (Gateway pale amani ) wangeuza kwa jumla DATA nchi jirani, isitoshe na hata wao wangeweza kupata DATA ya bure, sasa hivi wamebaki na hizo hizo 15% zao, mkiambiowa serikali haina uoni mnabisha !!! oneni hao wamrima wanataka kujipanga wazichukue tena zile 35 % za AIRTEL kwenye TTCL.....sie tumebaki na siasa tu na kupewa vijizawadi

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.