Habari za Punde

Uzinduzi wa Ujenzi Mradi wa Bwawani Mpya Zanzibar

Jengo la Hoteli ya Bwawani litakavyo kuwa baada ya kufanyiwa ujenzi wake na Muwekezaji Mzalendo na ujenzi wake utachukua karibu miezi 18 hadi kukamilika kwake ujenzi huo. 

Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, Mama Fatma Karume akizindua ujenzi huo kwa kuondoa kipasia kuashiria uzinduzi wake na kuonesha picha ya jengo litakavyokuwa baada ya kukamilika kwake, hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika katika ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Zanzibar.  
Mama Fatma Karume akifurahia picha ya Hoteli Mpya ya Bwawani baada ya kuzindua ujenzi huo baada ya kuondoa kipazia kuonekana mchoro wa jengo hilo litakavyokuwa. 
Mama Fatma Karume na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakiangalia picha ya jengo la Hoteli Mpya ya Bwawani wakati wa uzinduzi wa hoteli hiyo ya kisasa itakavyokuwa.
MC Farouk Abdulla akitowa historia ya Hoteli ya Bwawani wakati wa uzinduzi wa Ujenzi wa Bwawani Mpya uliofanywa na Mama Fatma Karume, katika ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.


Mama Fatma Karume akihutubia wakati wa hafla hiyo na kutowa nasaha zake kwa Wafanyabiashara na Wananchi wakati wa uzinduzi wa Ujenzi wa Bwawani Mpya.
Waalikwa katika uzinduzi huo wakifuatilia hutuba ya Mama Fatma Karume.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.