MATANGAZO MADOGO MADOGO

Tuesday, April 19, 2016

Hali Ilivyokuwa Katika Maeneo ya Mvua Ilionyesha Juzi na Kusababisha Kujaa kwa Maji Baadhi ya Maeneo ya Makaazi ya Wananchi Ikiwemo Eneo Hili la Tomondo Ziwa Maboga.

Waziri wa Kilimo Mifugo Uvuvi na Maliasili Mhe Hamad Rashid akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakati alipofika kuwafariji Wananchi wa Tomondo kwa kupa maafa ya kujaa kwa maji nyumba zao yaliosababishwa na Mvua za Masika zilizonyesha hivi karibuni. katika visiwa vya Zanzibar.
Mwananchi wa Tomondo akivushwa kwa kutumia beseni kwa ada ya shilingi 1000/= kuelekea upande wa pili. 


Wananchi wa Tomondo wakiwa katika boto wakipata msaada wa kuvushwa katika eneo hilo kwenda ngambu ya pili kutokana na kujaa kwa maji na nyumba nyingi kukumbu na hali hiyo.
Wananchi wa eneo la Tomondo ziwa maboga wakivushwa kwa kutumia boti kwa ada ya shilingi 1000/= kwa mtu mmoja kutokana na kujaa kwa maji katika eneo hilo.
Eneo la ziwa mabogo likiwa limefurika maji kutokana mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo ya Visiwa vya Zanzibar na kulata maafa kwa Wananchi wa maeneo yaliokumbwa maafa hayo.