Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Kambi ya Wananchi Waliopata Maafa ya Mvua Skuli ya Sebleni Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wananchi waliopata majanga ya kuingiliwa na maji katika nyumba zao wakati alipotembelea kambi maalum iliowekwa katika Skuli ya Sekondari ya Nyerere, alipofika kuwafariji na kuwapa pole na mtihani huo.
Baadhi ya Wananchi wa maeneo ya Nyerere, Kwahani Kwa Wazee na Sebleni wakiwa katika Kambi maalum ilioandaliwa kwa Wananchi waliopata maafa ya kuingiliwa na Maji Nyumba zao wakati wa mvua ilionyesha juzi jumapili katika maeneo ya Visiwa vya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwafariji Wananchi waliopata maafa ya mvua katika baadhi ya maeneo ya Visiwa vya Unguja, Katika Kituo hicho kuna Wananchi zaidi ya mia nne waliopata maafa hayo wakiishi kwa muda katika kituo hicho.
Balozi Seif Ali Iddi akiwatembelea Wananchi waliopata maafa ya mvua alipofika katika Kambi hiyo ilioandaliwa kwa ajili yao katika Skuli ya Sekondari ya Sebleni Zanzibar. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji Mtoto Rauthan Muhudin akiwa amebebwa na Mama yake Bi Kioni Mtumweni, wakati alipotembelea kambi hiyo na kuwafariji Wananchi hao waliopata mkasa wa kujaa kwa maji nyumba zao
Balozi Seif Ali Iddi akitembelea Kambi hiyo akiwa na Sheha wa Shehia ya Kwawazee.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimsiliza Afisa wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayotowa huduma ya kwanza kwa Wananchi hao K
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi msaada wa Vyakula vilivyotolewa na Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo la Amaan Zanzibar, wakati alipofika katika Kambi hiyo kuwafariji Wananchi hao.  

2 comments:

  1. serikali hamjipangi mwaka jana yalitokea hivihivi na mwakani itakuwa hivi hivi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sadakta wanauza sura tu na kutoa matamko ya kisiasa tu, mvua zikiptita halas

      Delete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.