Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wananchi
waliopata majanga ya kuingiliwa na maji katika nyumba zao wakati alipotembelea
kambi maalum iliowekwa katika Skuli ya Sekondari ya Nyerere, alipofika
kuwafariji na kuwapa pole na mtihani huo.
Baadhi ya Wananchi wa maeneo ya Nyerere, Kwahani Kwa Wazee na Sebleni wakiwa katika Kambi maalum ilioandaliwa kwa Wananchi waliopata maafa ya kuingiliwa na Maji Nyumba zao wakati wa mvua ilionyesha juzi jumapili katika maeneo ya Visiwa vya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwafariji Wananchi waliopata maafa ya mvua katika baadhi ya maeneo ya Visiwa vya Unguja, Katika Kituo hicho kuna Wananchi zaidi ya mia nne waliopata maafa hayo wakiishi kwa muda katika kituo hicho.
Balozi Seif Ali Iddi akiwatembelea Wananchi waliopata maafa ya mvua alipofika katika Kambi hiyo ilioandaliwa kwa ajili yao katika Skuli ya Sekondari ya Sebleni Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji Mtoto Rauthan
Muhudin akiwa amebebwa na Mama yake Bi Kioni Mtumweni, wakati alipotembelea
kambi hiyo na kuwafariji Wananchi hao waliopata mkasa wa kujaa kwa maji nyumba
zao
Balozi Seif Ali Iddi akitembelea Kambi hiyo akiwa na Sheha wa Shehia ya Kwawazee.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimsiliza Afisa wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayotowa huduma ya kwanza kwa Wananchi hao K
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi msaada wa Vyakula vilivyotolewa na Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo la Amaan Zanzibar, wakati alipofika katika Kambi hiyo kuwafariji Wananchi hao.
serikali hamjipangi mwaka jana yalitokea hivihivi na mwakani itakuwa hivi hivi
ReplyDeleteSadakta wanauza sura tu na kutoa matamko ya kisiasa tu, mvua zikiptita halas
Delete