Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani kufanyika tarehe 24/04/16

 Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumzia kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani yatakayofanyika Tarehe 24/04/2016 Zanzibar.

 Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akitoa hotuba kwa Waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusiana na Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani ambayo yatafanyika tarehe 24/04/2016 Zanzibar.Mwengine  ni Naibu Waziri wa Afya Harusi Idi.

Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akitoa ufafanuzi wa maswala mbalimbali yalioulizwa katika mkutano wake na Waandishi wa Habari akielezea kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani yatakayofanyika Tarehe 24/04/2016 Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.


Takwimu za Wizara ya Afya Zanzibar zinaonesha kwamba malaria imepungua kwa kiwango cha chini ya asilimia moja .
Aidha vifo vinavotokana na malaria pia vimepungua ambapo 2015 watu watatu tu walithibitishwa kufariki kwa malaria.

Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo Huko ofisini kwake alisema hayo ni Mafanikio makubwa ambayo sio rahisi kuyapata nchi nyengine ya Afrika.Alisema kwamba kazi ya kumaliza malaria si wajibu wa Wizara ya Afya peke yake ila ni wajibu wetu sote .

April 24 mwaka huu Wizara ya Afya imepanga kufanya matembezi ya hiari yatakayowajumuisha wananchi wote ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni 'Maliza Malaria Kabisa'

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.