Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Khalid Salum Mohammed (kulia) akikabidhiana Ofisi na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makame Mwadini leo katika ukumbi wa Tume ya Mipango Vuga Mjimkongwe wa Zanzibar baada ya uteuzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makame Mwadini akitoa shukurani kwa wafanyakazi wa tume ya mipango wakati wa makabidhiano ya Ofisi na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Khalid Salum Mohammed katika ukumbi wa Tume ya Mipango Vuga Mji Mkonge wa Zanzibar baada ya uteuzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makame Mwadini akiagana na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Khalid Salum Mohammed baada ya makabidhiano ya Ofisi katika viwanja vya Ofisi ya Tume ya Mipango leo Vuga Mji Mkongwe wa Zanzibar baada ya uteuzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
[Picha na Ikulu.]
STATE HOUSE
ZANZIBAR
OFFICE OF THE
PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 13.4.2016
WAZIRI wa Fedha na Mipango Mhe. Khalid Salum Mohammed amesema kuwa Tume ya
Mipango ina jukumu kubwa katika kufikia lengo na dhamira ya Serikali katika
kipindi hiki cha pili cha Awamu ya Saba katika kuongeza kiwango cha ukusanyaji
wa mapato sambamba na ukuaji wa uchumi.
Aliyasema hayo, mara baada ya
makabidhiano ya Ofisi ya Tume ya Mipango kati yake na Mhe. Dk. Mwinyihaji
Makame Mwadini, hafla iliofanyika katika
ukumbi wa Ofisi ya Tume hiyo iliyopo Vuga mjini Zanzibar na kuhudhuriwa
na baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na
Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyejiti wa Baraza la Mapinduzi.
Waziri Khalid akinukuu hotuba ya Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Kohamed Shein, aliyoitoa
Katika uzinduzi wa Baraza la Tisa la Baraza la Wawakilishi Dk. Khalid alisema
kuwa mafanikio katika ukusanyaji wa mapato na kasi ya ukuaji uchumi aliyoeleza
Rais itafikiwa kutokana na kujenga mashirikiano ya dhati kwa viongozi na wafanyakazi
wote.
“Malengo yote hayo mawili yatafikiwa
iwapo kutakuwa na mashirikiano ya kutosha likiwemo lengo la kuhakikisha kuwa
kasi ya ukuaji wa uchumi inafikia asilimia 8-10 katika miaka mitano ijayo na
lile la kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka TZS bilioni 362.8 mwaka
2014/2015 hadi kufikia TZS bilini 800 ifikapo mwaka 2020/2021”,alisema Dk. Khalid.
Katika maelezo yake Dk. Khalid
alisisitiza haja ya kufanya kazi kwa kujitolea kwa kila mfanyakazi na katika kila
sehemu aliyopo achape kazi kwani hayo ndio matarajio ya Mhe. Rais pamoja na
wananchi katika kuiletea Zanzibar maendeleo endelevu.
Waziri Khalid alisema kuwa rasilimali
fedha ni muhimu na sekta zote za Serikali zinategemea sana usimamizi na ugawaji
wa rasilimali hizo hivyo Tume ya Mipango ina jukumu kubwa katika kusimamia hilo
na kuhakikisha linafanikiwa.
Dk. Khalid aliahidi kuimarisha zaidi
mashirikiano kati yake, viongozi na watendaji wote wa Tume hiyo ambayo hapo
kabla ilikuwa chini ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala Bora kwa
lengo la kufikia matarajio ya wananchi katika kuwaletea maendeleo endelevu.
Aidha Waziri Khalid alimuhakikishia Mhe.
Dk. Mwinyihaji kuwa ataendelea kushirikiana nae samba na kuchota hazina ya
uzoefu, mawazo, busara na hekima alizonazo katika utendaji wake wa kazi huku
akiahidi kuwa hatoacha kujifunza kutoka kwa watendaji na viongozi wa Tume hiyo
ya Mipango.
Sambamba na hayo, Dk. Khalid alisisitiza
haja kwa viongozi na watendaji wa Tume hiyo kuimarisha zaidi mawasiliano
miongoni mwao pamoja na kupeana taarifa zilizosahihi.
Mapema Dk. Mwinyihaji Makame ambaye
katika Kipindi cha kwanza katika uongozi wa Awamu ya Saba alikuwa Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala
Bora aliwataka watendaji na viongozi wa Tume hiyo kutoa ushirikiano mkubwa kwa
Waziri huyo mpya kama walivyompa yeye katika uongozi wake.
Dk. Mwinyi aliwahakikishia watendaji wa
Wizara pamoja na Tume hiyo kuwa wamepata Waziri mchapa kazi na hodari na mwenye
kasi katika utendaji wake wa kazi hivyo wakimpa
mashirikiano ya kutosha anaamini kuwa mafanikio makubwa yatapatikana katika
kuiletea maendeleo Zanzibar.
Dk. Mwinyi alisema kuwa Tume ya Mipango
ndio roho ya nchi, kwani ndio inayotoa maelekezo ya matumizi na mipango yote ya
kifedha serikalini hivyo kuwepo mashirikiano katika uongozi wa Tume hiyo
kutafikia malengo yaliowekwa katika kuiimarisha Zanzibar.
Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya
watendaji wa Tume ya Mipango, Bi Sharifa
Abdalla Khamis aliahidi kuwa wafanakazio wote wa Tume hiyo watampa mashirikiano
makubwa Waziri wao huyo mpya huku wakiahidi kuongeza bidii katika utendaji wao
wa kazi.
Rajab Mkasaba,
Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024
2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment