Habari za Punde

Viongozi na wafanyakazi ofisi ya Rais na mwenyekiti wa BLM watakiwa kuendeleza mashirikiano


  
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar                                                             12.4.2016
---
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Ussi Gavu ameeleza haja kwa viongozi na wafanyakazi wa Wizara hiyo kuendeleza mashirikiano ya pamoja katika utendaji wao wa kazi ili kufikia lengo la Serikali la kuwatumikia na kuwahudumia wananchi wote.

Hayo aliyasema mara baada ya makabidhiano ya Ofisi hiyo yaliofanyika kati yake na aliyekuwa Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, hafla iliofanyika katika  ukumbi wa Ofisi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi iliopo Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Wizara hiyo.

Aidha Mhe. Gavu alieleza kuwa  mashirikiano ya pamoja yatafikia lengo katika kumsaidia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein la kuwaletea maendeleo wananchi wote.

Waziri huyo alitoa shukurani kwa Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein kwa kumteua kushika wadhifa huo na kuahidi kwa mashirikiano ya pamoja na viongozi pamoja na wafanyakazi wa Wizara hiyo lengo la Rais la kuiletea maendeleo Zanzibar litafikiwa.


Mhe. Gavu alieleza kuwa hakuna kubwa litakaloshinda iwapo kutakuwa na mashirikiano ya pamoja katika kutekeleza majukumu na wajibu sambamba na kufuata taratibu na sherika kwa kila mfanyakazi.

“Nimekuja hapa kwa ajili ya kufanya kazi hivyo sote tujiandae kwa kufanya kazi na kuendeleza mashirikiano yetu ili tumsaidia Mhe. Rais...” alisema Waziri Gavu.

Katika maelezo yake, Waziri Gavu alisisitiza haja wka wafanyakizi na viongozi wa Wizara hiyo kuwepo kwa mashirikiano na kuahidi kwa upande wake atatoa mashirikiano makubwa na kufanya kazi kwa kuelekezana na kushirikiana huku akiahidi kufanya kazi kwa taratibu na sheria za nchi zilizopo.

Waziri Gavu alitumia fursa hiyo kutoa shukurani kwa Dk. Mwinyihaji Makame kwa kuendelea kuwa na mashirikiano nae na kuahidi kuendelea kuchota mawazo na busara sambamba na hekima  kutoka kwake.

Mapewa Mhe. Dk. Mwinyihaji Makame alitoa pongezi kwa Waziri Gavu kwa kuteuliwa kuwa Waziri katika Wizara hiyo na kueleza kuwa hatua hiyo imekuja kutokana na utendaji wake wa kazi mzuri alioufanya katika Wizara yake ya zamani na imani yake ni kuwa katika wadhifa wake huo mpya atazidisha juhudi.

Dk. Mwinyihaji ambaye pia, ni Mwakilishi wa Jimbo la Dimani aliwataka wafanyakazi na viongozi wa Wizara hiyo kumpa mashirikiano makubwa Waziri huyo mpya kama walivyompa yeye wakati akiwa Waziri katika Wizara hiyo ambapo katika uongozi wake ilikuwa ni Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala Bora.

Aidha, Dk. Mwinyi alisisitiza haja kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa juhudi kubwa kama wanavyosisitiza viongozi wakuu hapa nchini akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Johm Pombe Magufuli pamoja na Dk. Shein ili kuendelea kuiletea maendeleo Zanzibar.

Dk. Mwinyi alitoa shukurani kwa Dk. Shein kwa kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu uliopita na kutoa pongezi za pekee kwa Ofisi ya Faragha ya Mhe. Rais kwa mashirikiano waliyompa huku akimuomba Waziri huyo mpya kuwatumia wafanyakazi wa Ofisi hiyo katika utendaji wake wa kazi.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wafanyakazi wa Wizara hiyo, Katibu wa Rais Haroub Shaib Mussa alitoa pongezi kwa viongozi hao wote katika utendaji wao wa kazi sambamba na kuwa karibu na wafanyakazi pamoja na wananchi wa Majimbo yao.

Katibu Shaibu alimuahidi Waziri Gavu kuwa wafanyakazi wa Wizara hiyo wataendelea kumpa mashirikiano makubwa na kuendelea kumuunga mkono katika utendaji wake wa kazi kwa lengo moja la kuwaletea wananchi wa Zanzibar maendneleo endelevu.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.