Habari za Punde

Balozi Seif Ali Atembelea Miradi ya Ujenzi wa Mitaro Mnazi Mmoja na Jangombe kwa Bint Hamrani.

Uwanja wa Mnazi Mmoja ukiwa umejaa maji kutokana na mvua za masika zilizonyesha juzi. na kuleta madhara katika maeneo mbalimbali ya Visiwa vya Unguja kujaa kwa maji.  
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipata maelezo ya ujenzi wa Mradi wa Mtaro wa Maji katika Uwanja wa Mpira wa Mnazi Mmoja wakati wa ziara yake kutembelea miradi hiyo inayotarajiwa kuondoa kero ya kujaa kwa maji katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi akizungumza wakati wa ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alipofika katika maeneo ya Uwanja wa Mpira Mnazi Mmoja kuangalia maendeleo ya Mradi huo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,akimzikiliza Mkurugenzi wa Michiri wa Baraza la Manispa Zanzibar Mzee Abdalla akitowa maelezo ya ujenzi wa Mtaro ya Maji Machafu wa Mnazi Mmoja wakati wa ziara ya Balozi Seif Ali Iddi kutembelea miradi hiyo. 
Balozi Seif Akizungumza na Watendaji wa Baraza la Manispa wakati wa ziara yake, kutembelea Miradi hiyo ya kuondoa kero za Wananchi katika kujaa kwa maji ya mvua katika maeneo ya makaazi yao. 
Mkurugenzi wa Idara ya Michiri Baraza la Manispa Mzee Abdalla akitowa maelezo na kuonesha eneo uliopita mtaro wa maji katika eneo la Jangombe kwa Bint Hamrani wakati wa ziara ya Balozi Seif Ali Iddi kutembelea miradi hiyo. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika eneo lililopita mtaro wa maji kuondoa kero kwa Wananchi wa Jangombe wanakumbwa na mafuriko wakati wa msimu wa mvua za masika. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.