TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
MCT
yatangaza majina ya wateule wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania
(EJAT) 2015
·
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora, Tom Nyanduga kuwa Mgeni Rasmi
Kamati
ya maandalizi ya EJAT 2015 leo limetangaza majina 84 ya wateule wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari
Tanzania (EJAT) 2015. Idadi hiyo ni ongezeko la wateule 31 ukilinganisha na
tuzo za 2014 ambapo wateule walikuwa ni 53 tu.
Pia kamati imeeleza kuwa Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tom Bahame Nyanduga ndio Mgeni
Rasmi kwenye Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT ) 2015 zitakazofanyika kwenye tamasha la usiku la
utoaji wa tuzo hizo Aprili 29, 2016 ,
Dar es Salaam.
Kutangazwa kwa wateule wa EJAT 2015 kunafuatia
kukamilika kwa kazi ya kuzipitia na kuchagua zile zilizo na ubora zaidi iliyofanywa
na jopo la majaji 10 lililokaa mwezi Machi mwaka huu. Majaji hao ambao ni
wataalamu mbalimbali wa masuala ya habari walipitia kazi za kiandishi zaidi ya 570
zilizowasilishwa kwenye makundi ya kushindaniwa 22 kwenye tuzo za Umahiri wa
Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2015.
Ripoti ya jopo la majaji hao kuhusu
wateule wa EJAT 2015, inaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa kwa wateule kwa upande wa luninga ambapo kuna
wateule 27 kutoka wateule wawili katika
tuzo za 2014. Pia kuna ongezeko kwenye wateule wa redio kutoka 17 hadi 27. Hata
hivyo kwa upande wa magazeti wateule wamepungua kidogo kutoka wateule 34 wa
tuzo za 2014 hadi 32 kwa tuzo za mwaka 2015.
Idadi ya wateule wanawake pia
imeongezeka kufikia 28 kutoka wateule 18 kwenye tuzo za EJAT 2014. Pia ripoti inaonyesha kuongezeka kwa kazi zilizoletwa
na redio za kijamii mwaka huu ambapo baadhi yao zimeweza kutoa wateule kwenye
tuzo za EJAT 2015.
Jopo hilo la majaji liliongozwa na
mwenyekiti wake, Bi. Valerie Msoka, wajumbe wengine walikuwa Dk. Joyce Bazira Ntobi ambaye alikuwa katibu
wa jopo, na Ali Uki. Wanajopo wengine
walikuwa Jesse Kwayu, Kiondo
Mshana, Juma Dihule, Godfrey Nago, Nathan Mpangala na Pili Mtambalike. Waandishi hao 84 wataingia
kwenye kinyang’anyiro cha mashindano ya EJAT 2015.
Majaji hao 10 waliapishwa na Rais wa
Baraza la Habari Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo Machi 11, 2016 kabla ya
kuanza kazi hiyo. Hii itakuwa ni mara ya
saba kuwatuza waandishi waliofanya vizuri katika kazi zao za kiuandishi chini
ya utaratibu wa EJAT.
Sambamba na EJAT, Jopo la wataalam kwa
ajili ya Tuzo ya Maisha ya Mafanikio katika Uandishi wa Habari (LAJA) umeanza
kazi ya kutafuta mteule wa tuzo hiyo kwa mwaka huu ambae atatangazwa wakati wa
Tamasha hilo la usiku. Jopo la LAJA
linalongozwa na Mwenyekiti wake Bi. Lilian Kallaghe lina wajumbe watano ambao
ni pamoja na Hamis Mzee, Fili Karashani, Joseph Kulangwa na Wenceslaus Mushi.
Makundi yaliyoshindaniwa
ni yafuatayo:
1. Tuzo ya Uandishi wa Habari za
Uchumi na Biashara
2. Tuzo ya Uandishi wa Habari za
Michezo na Utamaduni
3. Tuzo ya Uandishi wa Habari za
Mazingira
4. Tuzo ya Uandishi wa Habari za
Afya
5. Tuzo ya Uandishi wa Habari za
VVU/Ukimwi
6. Tuzo ya Uandishi wa Habari za
Watoto
7. Tuzo ya Uandishi wa Habari za
Utawala Bora
8. Tuzo ya Uandishi wa Habari za
Jinsia
9. Tuzo ya Uandishi wa Habari za
Sayansi na Teknolojia
10 Tuzo ya Uandishi wa Habari za
Uchunguzi
11. Tuzo ya Uandishi wa Habari za
Afya ya Mama na Mtoto
12. Tuzo ya Uandishi wa Habari za
Elimu
13. Tuzo ya Uandishi wa Habari za
Utalii na Uhifadhi
14. Tuzo ya Uandishi wa Habari za
Watu Wenye Ulemavu
15. Mpiga Picha Bora – Magazeti
16. Mpiga Picha Bora – Runinga
17. Mchora Katuni Bora
18. Tuzo ya Uandishi wa Habari za
Kilimo
19. Tuzo ya Afya ya Uzazi kwa vijana
20. Tuzo ya Uandishi wa Habari za
Gesi, Mafuta na Uchimbaji Madini
21. Tuzo ya Uandishi wa Habari za
Manunuzi ya Umma
22. Tuzo ya Uandishi wa Habari za
Kodi na Ukusanyaji Mapato
Ifuatayo ni orodha ya wateule wa
EJAT 2015 ambao wanatoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari
WATEULE WA
EJAT 2015
SN
|
JINA LA
MWANDISHI
|
CHOMBO
CHA HABARI
|
MKOA
ANAOTOKA
|
1.
|
Sylvester Joseph
|
Afya
Radio
|
Mwanza
|
2.
|
Fatuma Mtengamani
|
Ulanga FM
|
Ulanga-Mahenge
(Morogoro)
|
3.
|
Adam Hhando
|
CG FM
|
Tabora
|
4.
|
Abisae Maeda
|
TV1/Kilimanjaro
Film Institute
|
Arusha
|
5.
|
Mwashamba Juma
|
Zanzibar
Leo
|
Zanzibar
|
6.
|
Jackline Masinde
|
Mwananchi
|
DSM
|
7.
|
Peter Rodgers
|
ITV
|
Mwanza
|
8.
|
Lucas Maziku
|
Star TV
|
Mwanza
|
9.
|
Maajabu Madiwa
|
Pangani
FM
|
Pangani-Tanga
|
10.
|
Ezekiel Kamanga
|
BBC &
Bomba FM
|
Mbeya
|
11.
|
Malongo Mbeho
|
Metro FM
|
Mwanza
|
12.
|
Annastazia Maginga
|
Raia
Tanzania
|
Mwanza
|
13.
|
John
Leon Lewanga
|
TBC
|
DSM
|
14.
|
Mussa Kinkaya
|
Sunrise FM
|
Arusha
|
15.
|
Victor Makwawa
|
Dodoma FM
|
Dodoma
|
16.
|
Pili Mlindwa
|
Pangani
FM
|
Pangani-Tanga
|
17.
|
Zulfa Golay
|
Mwananchi
|
Arusha
|
18.
|
Tumaini Msowoya
|
Mwananchi
|
Iringa
|
19.
|
Nuzulack Dausen
|
The
Citizen
|
DSM
|
20.
|
Haji Mohamed
|
Zanzibar
Leo
|
Pemba-Zanzibar
|
21.
|
Silvano Kayera
|
Mlimani
|
DSM
|
22.
|
Christian Msafiri
|
CG FM
|
Tabora
|
23.
|
Grace Mbise
|
Bomba FM
|
Mbeya
|
24.
|
Salome Kitomari
|
Nipashe
|
DSM
|
25.
|
Kelvin Matandiko
|
Mwananchi
|
DSM
|
26.
|
Mansour Jumanne
|
SAUT FM
|
Mwanza
|
27.
|
Frank Bahati
|
TBC1
|
DSM
|
28.
|
Khamis Suleiman
|
Channel
Ten
|
DSM
|
29.
|
Emmanuel Buhohela
|
ITV
|
DSM
|
30.
|
Lusekelo Philemon
|
The
Guardian
|
DSM
|
31.
|
John Nsuza
|
TV1
|
Arusha
|
32.
|
Esther Zelamula
|
Channel
ten
|
DSM
|
33.
|
Elibahati Akyoo
|
TV1/ Kilimanjaro Film Institute
|
Arusha
|
34.
|
Idd Juma
|
Afya
Radio
|
Mwanza
|
35.
|
Mashaka Mgeta
|
The
Guardian
|
DSM
|
36.
|
Kisali Simba
|
Star TV
|
Shinyanga
|
37.
|
Editha Kinyaiya
|
TV1/Kilimanjaro Film Institute
|
Arusha
|
38.
|
Emmanuel Kitomari
|
TV1/Kilimanjaro Film Institute
|
Arusha
|
39.
|
Maulid kambaya
|
Radio One
|
DSM
|
40.
|
Lulu George
|
Nipashe
|
Tanga
|
41.
|
Mussa Siwayombe
|
Mwananchi
|
Arusha
|
42.
|
Victor Eliah
|
TBC
|
DSM
|
43.
|
Cassius Mdami
|
Channel
Ten
|
DSM
|
44.
|
Anthony Masai
|
Triple A
FM
|
Arusha
|
45.
|
Temigunga Mahondo
|
Radio
Country FM
|
Iringa
|
46.
|
Beatrice Shayo
|
Nipashe
|
DSM
|
47.
|
Rahma Suleiman
|
Nipashe
|
Zanzibar
|
48.
|
Haika Kimaro
|
The
Citizen
|
DSM
|
49.
|
Halfan Lihundi
|
ITV
|
Arusha
|
50.
|
Lydia Igarabuza
|
EATV
|
DSM
|
51.
|
Valeria Mwalongo
|
Tumaini
|
DSM
|
52.
|
Peninah Kajura
|
HHC Radio
|
Mwanza
|
53.
|
Goodluck Mvamba
|
SAUT FM
|
Mwanza
|
54.
|
Said Michael
|
Mtanzania
|
DSM
|
55.
|
Abdul Kingo
|
Nipashe
|
DSM
|
56.
|
Nora Damian
|
Mtanzania
|
DSM
|
57.
|
Sauli Gilliard
|
The
Citizen
|
DSM
|
58.
|
Alfayo Misiyeki
|
TV1/Kilimanjaro Film Institute
|
Arusha
|
59.
|
Samson Kapinga
|
TV1/ Kilimanjaro Film Institute
|
Arusha
|
60.
|
Florence Majani
|
Mwananchi
|
DSM
|
61.
|
Selemani Mkufya
|
TBC1
|
DSM
|
62.
|
Kasilda Mgeni
|
Star TV
|
Morogoro
|
63.
|
Tuma Dandi
|
Mlimani
|
DSM
|
64.
|
Eveline Mhozya
|
CG FM
|
Tabora
|
65.
|
Vivian Pyuza
|
CG FM
|
Tabora
|
66.
|
Joseph Mwendapole
|
Nipashe
|
DSM
|
67.
|
Hadija Jumanne
|
Mwananchi
|
DSM
|
68.
|
Christina Mwakangale
|
Nipashe
|
DSM
|
69.
|
Sanula Athanas
|
Nipashe
|
DSM
|
70.
|
Mwanahiba Richard
|
Mwanaspoti
|
DSM
|
71.
|
Japhary Ramadhan
|
ABM FM
|
Dodoma
|
72.
|
Bernard Lugongo
|
The
Citizen
|
DSM
|
73.
|
Emmanuel Mollel
|
TV1/ Kilimanjaro Film Institute
|
Arusha
|
74.
|
Joel Ulomi
|
Arusha
One
|
Arusha
|
75.
|
Haji Nassor
|
Zanzibar
Leo
|
Chake Chake-Pemba
|
76.
|
Peti Siyame
|
Habari
Leo
|
Sumbawanga-Rukwa
|
77.
|
Robert Okanda
|
Dailynews
|
DSM
|
78.
|
Nuru Hassan
|
Afya
|
Mwanza
|
79.
|
Shija Felician
|
The
Citizen
|
Kahama
|
80.
|
Salum Maige
|
Mwananchi
|
Geita
|
81.
|
Projestus Binamungu
|
Star TV
|
Mwanza
|
82.
|
Regina Kulindwa
|
Afya
|
Mwanza
|
83.
|
Denis Nyali
|
Nuru
|
Iringa
|
84.
|
Sam Mahela
|
ITV
|
DSM
|
Waandaaji wa EJAT 2015 ni pamoja na Mfuko
wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa
Afrika- Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake
Tanzania (TAMWA), Jukwaa la Wahariri (TEF), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya
Habari (MOAT), Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), Chama cha
Waandishi wa Habari Walio katika Mapambano Dhidi ya UKIMWI Tanzania (AJAAT),
Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), PSI-Tanzania,
Unicef, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Haki Elimu, SIKIKA, Evidence
for Action, Amref Health Africa na BESTDialogue/ANSAF.
Kajubi D.
Mukajanga
Mwenyekiti
Kamati ya
Maandalizi ya EJAT 2015
No comments:
Post a Comment