Habari za Punde

Tunaweza Kuimaliza Malaria -JK

Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akielezea  juhudi zilizofanywa na  serikali ya Tanzania katika kuukabili ugonjwa wa malaria, ilikuwa wakati wa hafla ya miaka 10 ya Malaria no More iliyofayika jana alhamis New York Marekani, Mhe. Kikwete amealikwa katika hafla hiyo   kutokana na mchango wake mkubwa katika pamoja na  mengin kuwahamasisha viongozi wa Afrika kuongeza juhudi za kisera, kimkakati na bajeti  hali ambayo imechangia sana katika  kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano. pamoja naye ni  Bw. Peter Chernin, Bw. Ray Chambers na mwezeshaji,  Bw. Wolft Blitzer wa CNN.
Mwanzilishi wa  Malaria no More, Bw Peter Chernin akimkabidhi Mhe. Rais Mstaafu, Kikwete  tuzo ya White House Summit Awards ikiwa ni kutambua na kuthamin mchango na uongozi wake katika jitihada za kuukabili  ugonjwa wa malaria, wengine waliopewa tuzo hiyo ni Bw. Ray Chambers na Kampuni ya  Sumitomo Chemical  ambayo imejenga kiwanda cha vyandarua cha A-Z Arusha Tanzania.
Sehemu  ya Wageni zaidi ya 250 kutoka masharika na makampuni mbalimbali  ambako ni sehemu ya wadau wa kubwa wanaochangia juhudi za kutokomeza na kudhibiti ugonjwa wa malaria
Mhe Rais Mstaafu akiwa na Bw. Ray Chambers na Mkewe Bi. Patti Chambers muda  mfupi kabla ya  hafla ya kuanza.
 Mhe Kikwete akiwa na  Bw Blitzer mtangazaji maarufu wa CNN kupitia kipindi chake cha  Situation Room
Mhe. Kikwete akiwa na  sehemu ya wageni wakipata picha
Mhe Kikwete akiwa na ujumbe wake kutoka  kushoto ni Bw. Togolan Mavula,  Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na Professa Mohamed Janabi
Mhe. Rais Mstaafu katika mkutano na Bodi mpya ya Malaria no More muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya miaka 10 ya Malaria No More

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.