Habari za Punde

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo Akabidhi Mashine ya OXYGEN na Kutembelea Kambi ya Kipindipindu Chumbuni Unguja.

Muunguzi wa hospitali ya wazazi ya Muembeladu Ruzuna Abdulrahman akimkaribisha Waziri wa Afya Mhe.Mahmoud Thabit Kombo wakati wa hafla ya kukabidhiwa mashine ya Oxygen iliotolewa na Kampuni ya GSM ya mjini Dar es Salaam kwa ajili ya Hospitali hiyo.
 Mwakilishi  wa Kampuni ya GSM Doris Molel akimkabidhi Waziri wa Afya Mhe.Mahmoud Thabit Kombo mashine ya Oxygen kwa ajili ya matumizi ya Watoto Njiti wanaozaliwa katika Hospital ya Muembeladu Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Mahmoud Thabit Kombo akiishukuru Kampuni ya GSM ya Dar es Salaam kwa kutoa msaada wa mashine ya Oxygen kwa ajili ya Watoto njiti wanaozaliwa katika Hospitali ya Muembeladu Mjini Zanzibar.
Mkuu wa kambi ya kipindupindu iliopo Mtaa wa Chumbuni Dkt. Ramadhan mikidadi akimkarisha Waziri wa Afya Mahamoud Thabit Kombo, Naibu Waziri Harusi Said Suleiman (kulia) na Mwakilishi wa Kampuni ya GSM walipotembelea kambi hiyo
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahamoud Thabit Kombo  akitembelea mahema ya wagonjwa wa Kipindupindu katika kambi iliopo Chumbuni Zanzibar.


MAHEMA yanayolazwa wagonjwa wa Kipindupindu katika kambi ya Mtaa wa Chumbuni. (PICHA NA ABDALLA OMAR HABARI- MAELEZO).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.