Habari za Punde

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhub Afungua Mkutano wa Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi katika Nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika Leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua mkutano kuhusu kuwezesha wanawake kiuchumi katika nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika. Mkutano huo umeandaliwa na Jopo la Ngazi ya Juu la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon alilolituewa Mwanzoni mwa huu, kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekezo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwezesha wanawake kiuchumi ifikapo 2030. uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Hyatt Hotel Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Jopo la ngazi ya Juu la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kuwezesha wanawake kiuchumi Baada ya kufungua mkutano kuhusu kuwezesha wanawake kiuchumi katika nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika. Mkutano huo unazungumzia kuhusu kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekezo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwezesha wanawake kiuchumi ifikapo 2030. Umefanyika Leo April 29,2016. (Picha na OMR)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.