Habari za Punde

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe Riziki Pembe Azungumza na Waliku Wakuu wa Skuli za Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe, Naibu Waziri Mhe Mmanga Mjawili na Naibu Katibu Mkuu Ndh Abdalla Mzee wakiwasikiliza Walimu Wakuu wa Skuli za Msingi na Sekondari za Mkoa wa Mjini Magharibi wakielezea matatizo yao katika Skuli zao hasa katika kipindi hichi za mripuko wa maradhi ya matumbo, mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Haile Sselassie Zanzibar. 
Walimu Wakuu wakitowa maelezo ya Skuli zao wakati wa Mkutano na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma, kueleza matatizo ya Skuli zao na jinsi ya kuyatatua matatizo hayo.  

Mwalimu Mkuu wa Skuli za Mkoa wa Mjini Magharibi akisisitiza jambo wakati wa Mkutano huo.
Mwalimu Mkuu akitowa matatizo ya Skuli yake wakati wa Mkutano na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar katika ukumbi wa Skuli ya Haile Zanzibar. 


Walimu Wakuu wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano na Waziri wa Elimu Zanzibar. wakifuatilia michango ikitolewa na Walimu Wakuu wa Skuli mbalimbali za Sekondari na Msingi katika kipindi hichi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.