Habari za Punde

Wafugaji wa Nyuki Pemba Wakabidhiwa Vifaa vya Kuvunia Nyuki na Kufuga

Masanduku maalumu ya mbayo ni mitego ya kisasa 54, kwa ajili ya kutegea nyuki, iliotolewa na Idara ya mazingira Zanzibar, ambapo juzi ilikabidhiwa kwa vikundi vya ufugaji nyuki 11 vya kisiwani Pemba, zoezi lililofanywa na Mkurugenzi wa Idara hiyo Zanzibar Juma Bakar Alawi ‘JB’ hafla iliofanyika Machomane Chakechake Pemba

Watendaji wa Idara ya Mazingira Pemba wakipanga panga vifaa vya kuvunia asali, ambavyo baadae vifaa hivyo pamoja na mitego 54 ilikabidhiwa kwa wanavikundi 11 vya ufugaji wa nyuki kisiwani Pemba, hafla iliofanyika Machomane Idara ya mazingira,
Mratibu wa Mradi wa Uimarishaji wa Mazingira na mabadiliko Tabianchi Zanzibar Sudi Mohamed Juma, akitoa maelezo ya mradi huo, mbele ya wanavikundi 11 ya ufugaji nyuki Kisiwani Pemba, kabla ya wanavikundi hao kukabidhiwa mitego ya nyuki na vifaa vya kuvunia asali, hafla iliofanyika Machomane Chakechake Pemba,
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Zanzibra Juma Bakar Alawi ‘JB’ akimkabidhi vifaa vya kuvunia asali na viatu maalumu mwanakikundi wa Jumuia ya wanawake Tundauwa ‘JUMATU’ Raya Abdalla Rashid ambapo vikundi 11 vilikabidhiwa vifaa hivyo ikiwemo masandukua maalumu matano kila kikundi ya kutegea nyuki. 
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Zanzibra Juma Bakar Alawi ‘JB’ akimkabidhi vifaa vya kuvunia asali na viatu maalumu mwanakikundi cha ‘MTAJI WA MASKINI’ cha Kwazani Wambaa, ambapo vikundi 11, vilikabidhiwa vifaa hivyo ikiwemo masanduku maalum matano kila kikundi ya kutegea nyuki.
Mwanakikundi cha ufugaji nyuki cha ‘Nia njema’ cha Tumbe Mashariki, akibeba sanduku maalumu kwa ajili ya kufugia nyuki ambayo mitego hiyo 54, iliotolewa kwa vikundi 11 kisiwani Pemba na Idara ya Mazingira Zanzibar, hafla iliofanyika Machomane Chakechake
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Zanzibra Juma Bakar Alawi ‘JB’ akimkabidhi masanduku maalumu kwa ajili ya mitego ya nyuki kwa mwanakikundi wa ‘GPEC’ kutoka Mwambe, ambapo vikundi 11 vilikabidhiwa masanduku hayo pamoja na vifaa maalumu ya kuvunia asali. 
Mkurugenzi wa Idara hiyo Zanzibar Juma Bakar Alawi ‘JB’, akiwa katika picha ya pamoja na Wafugaji wa Nyuki Kisiwani Pemba hafla iliofanyika Machomane Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.