Rais John Pombe Magufuli akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kudhamini mkutano wa Dodi ya Makandarasi Nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB Corporate, Fank
Nyabundege. Anayetazama kati kati ni Mwenyekiti
wa Bodi ya Makandarasi (CRB)
Eng. Consolata Ngimbwa akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda.
Rais John Pombe Magufuli akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kudhamini mkutano wa Bodi ya Makandarasi Nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB Corporate, Fank Nyabundege. Anayetazama kati kati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi (CRB) Eng. Consolata Ngimbwa akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya Mikopo wa Benki ya TIB Corporate, Theresia Soka akimweleza mmoja wa makandarasi kuhusu huduma zinazotolewa na benki yake. Anayetazama kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa benki ya TIB Corporate, Bahati Minja.
Benki
ya TIB Corporate imepongezwa na wadau mbalimbali juu ya mpango wake wa
kuwawezesha kifedha makandarasi wa ndani ili waweze kutekeleza vema majukumu
yao ya kikandarasi.
Akizungumza
wakati wa mkutano wa mashauriano wa mwaka wa bodi ya makandarasi, Kaimu Msajili
wa Bodi ya Makandarasi nchini (CRB), Rhoben Nkori alisema anaipongeza
benki ya TIB Corporate kwa kukubali kuwapa makandarasi mikopo na udhamini bila
gharama zozote kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali.
‘Bodi
ya Makandarasi (CRB) imeingia makubalinao na benki ya TIB Corporate ili iweze
kutoa mikopo baada tu ya kupata barua kutoka bodi ya makandarasi’ alisema bwana
Nkori.
Mkutano
huo wa mashauriano na maonyesho wa bodi ya makandarasi mwaka huu una dhima ya,
‘Mpango wa makusudi wa kuwajengea uwezo wa kiuchumi endelevu wakandarasi
wazalendo, Changamoto na mustakabali wake’.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya TIB Corporate, Frank Nyabundege amesema kama benki
inayomilikiwa na serikali inaunga mkono moja kwa moja juhudi za serikali za kuwawezesha
makandarasi ili waweze kushiriki katika kukuza uchumi.
‘Tumeona
juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuwawezesha wakandarasi wazalendo,
kwa kuanza kuwapa miradi mikubwa, ndio maana tumeanzisha huduma mbalimbali za
kibenki kama dhamana ya kibenki bila gharama yoyote pamoja na mkopo wa ununuzi
wa vifaa ambazo zitawasaidia wakandarasi wa ndani kufanikisha miradi yao bila
usumbufu wowote’ alisema bwana Nyabundege.
No comments:
Post a Comment