Habari za Punde

Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) Yaangamiza Tani 42.2 ya Bidhaa Mchanganyiko Zilizoharibika na Zile Zisizoruhusiwa kwa Matumizi ya Binaadamu

Wafanyakazi wa ZFDB wakipakia shehena ya bidhaa zilizoharibika tayari kwenda kuangamizwa katika Dampo la Kibele Mkoa Kusini Unguja.
Bidhaa mbali mbali zilizoharibika zikiteremshwa kutoka kwenye gari na wafanyakazi wa Bodi ya chakula na Vipodozi katika Dampo la Kibele kwa ajili ya kuangamizwa.
Mkuu wa Idara ya Usalama na Ubora wa chakula wa ZFDB Aisha Suleiman Mubandakazi akizungumza na waandishi wa habari juu ya zoezi la kuangamiza bidhaa mbali mbali zilizoharibika na zilizokatazwa kwa matumizi ya binadamu.
Burdoza la Manispaa ya Zanzibar likiwa kazini kuangamiza bidhaa hizo katika eneo la Kibele Mkoa Kusini Unguja.
Wafanyakazi wa ZFDB wakiongozwa na Mkuu wa operesheni ya uangamizaji bidhaa zilizoharibika Abdulaziz Shaib Mohamed (katikati) mwenye shati wakifuatilia uangamizaji wa bidhaa hizo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.