Habari za Punde

Dk Shein: WanaCCM endelezeni vuguvugu la ushindi hadi 2020

STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                        30 Mei, 2016
---

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi 

ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa Chama cha 

Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein amewataka 

wanachama na wapenzi wa chama hicho kisiwani Pemba 

kuendeleza vuguvugu la ushindi wa chama hicho hadi 

uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.

Dk. Shein amesema vuguvugu hilo halina budi kwenda 

sambamba na usimamizi makini wa utekelezaji wa Ilani ya 

Uchaguzi ya Chama hicho ya 2015/2020 ambayo ndio 

chachu ya ushindi wa CCM katika uchaguzi wa marudio 

uliofanyika mwezi Machi 2016.

Dk. Shein amesema hayo leo wakati alipokuwa 

akizungumza na viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya 

mashina hadi wilaya wa wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini 

Pemba.

“Kazi ya chama cha siasa wakati wote ni kuendeleza 

vuguvugu la kisiasa mbalo litawaweka wanachama na 

wapenzi wake pamoja kwa lengo la kuimarisha uhai wake 

na kujipambanua katika kutekeleza malengo yake kwa jamii” 

Dk. Shein alisisitiza.

Aliwaeleza viongozi hao kuwa kazi kubwa inayowakabili 

wana CCM na wananchi ni “kutekeleza Ilani” na kuangalia 

namna gani serikali itafanya kazi kwa kutekeleza Ilani hiyo.

Dk. Shein aliwapongeza na kuwashukuru viongozi hao kwa 

kusimama imara na kwa ujasiri mkubwa hadi CCM ikaibuka 

na ushindi wa kishindo kwa mgombea wake wa urais huku 

ikikomba viti vyote vya uwakilishi na udiwani Unguja na 

Pemba.
Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM Zanzibar 

aliwakumbusha viongozi hao kuwa mwaka ujao chama 

hicho kitafanya uchaguzi wake kuwapata viongozi hivyo 

hawana budi kuanza kujiandaa. 

“Ni uchaguzi utakaoimarisha chama chetu kwa kupata 

viongozi makini na wenye uwezo wa kukiongoza chama 

chetu na kutuletea ushindi katika uchaguzi wa 20202” Dk. 

Shein alieleza na kuwasisitizia viongozi hao kuwa sasa ni 

kazi tu hakuna kulala. 

Katika hatua nyingine Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM 

aliwaeleza viongozi hao kuwa chama hakitawavumilia 

viongozi ambao hawatatimiza majukumu yao hivyo 

kuwatanabahisha viongozi katika chama hicho kuepuka 

ubabaishaji.

Dk. Shein yuko kisiwani Pemba wa ziara ya siku tatu 

kuwashukuru wanachama na wapenzi wa chama hicho kwa 

ushindi mkubwa walioupata katika uchaguzi mkuu uliopita.Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.