Mkuu wa Idara ya macho kutoka Hospitali ya Jimbo la Jiangsu Nchini China Dkt. Liu Qing Huai akitoa mafunzo kwa madaktari wa vitengo vya macho, matumbo ya akinamama na saratani wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja katika kuwajengea uwezo wafanyakazi hao.
Waandishi wa Habari wakipata maelezo kutoka kwa Dkt. Liu Qing Huai kuhusu mafunzo wanayotolewa kwa wafanyakazi wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.
Picha na Miza Othman -Maelezo Zanzibar.
Na Maryam Kidiko -Maelezo Zanzibar.
Mkuu wa Kitengo cha macho Dkt Slim Moh’d Mgeni amesema jumla ya wagojwa 70 wanaosumbuliwa na matatizo ya macho kutoka Zanzibar wanatarajiwa kupatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Mnazi mmoja.
Akizumgumza na waandishi wa habari huko hospitali ya Mnazi mmoja, DKT. Slim amesema wagojwa watakaofanyiwa matibabu hayo ni watu wazima pamoja na wenye magojwa ya kinamama yakiwemo kensa ya kizazi.
Amesema matibabu hayo yatafanywa kwa ushirikiano na madaktari bingwa kutoka China ambao wamekuja maalum kwa kazi hiyo wakiwa na vifaa vya kisasa vya upasuaji.
Ameongeza kuwa matibabu hayo yatatolewa bure kwa wananchi wote na kuwataka wale wenye matatizo hayo waende Hospitali ya Mnazimmoja ili kupatiwa matibabu.
Nae Msaidizi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Dkt. Munir Abdalla Moh’d amesema madaktari hao wamekuja kwa lengo la kutoa mafunzo kwa madakatari wa vitengo vya magonjwa ya macho na magonjwa ya wanawake.
Aidha amesema madaktari hao ambao watakuwepo nchini kwa muda wa wiki moja watashuhulikia zaidi kesi ngumu zinazo hitaji upasuaji .
Nae Daktari bingwa wa macho kutoka Hospitali ya Jimbo la Jiangsu Dkt. Liu Qing Huai amesema lengo la kutoa mafunzo kwa wataalamu wa kitengo cha macho Zanzibar ni kuwajengea uwezo ili waweze kukabiliana na matatizo hayo ambayo yamekuwa yakiwasumbua wananchi wengi hasa wanapoingi hatua ya uzee.
No comments:
Post a Comment