Habari za Punde

Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Chaadhimisha Miaka 24..

Watendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba wakiwa na watoto ambao ni wanachama wa Jumuiya watu wenye ulemavu wa akili Pemba, pamoja na waalimu, mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya miaka 24 ya ZLSC yaliofanyika uwanja wa Gombani Chakechake, 
Mjumbe wa kamati tendaji wa Jumuiya kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa akili Zanzibar Mkubwa Hamad Omar, akielezea jinsi watu wa jumuia yake wanavyoweza kuleta mafanikio nadani ya jamii, kwenye maadhimisho ya miaka 24 ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, yaliofanyika uwanja wa Gombani Chakechake
Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed akimkabidhi kepteni wa timu ya vijana wenye ulemavu wa akili Pemba zawadi Maulid, mara baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi, kwenye maadhimisho ya siku ya kutimia miaka 24 ya ZLSC yaliofanyika uwanja wa Gombani,
Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed akimkabidhi mshindi wa mbio za mbatata kijana mwenye ulemavu wa akili Pemba, mara baada ya kuibuka na mshindi, kwenye maadhimisho ya kutimia miaka 24 ya ZLSC, yaliofanyika uwanja wa Gombani
Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba Fatma Khamis Hemed, akimkabidhi Riziki Juma Khami mwenye ulemavu wa akili, zawadi ya kuwa mshindi wa kula maandazi, kwenye maadhimisho ya miaka 24 ya ZLSC yaliofanyika uwanja wa Gombani
 Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Safia Saleh Sultan akimkabidhi mmoja wa wanachama wa Jumuia kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa akili Pemba, zawadi za Jumuia hiyo, ambapo hafla hiyo iliambatana na maadhimisho ya miaka 24 ya ZLSC, na kufanyika uwanja wa Gombani Chakechake
Watendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, wakiwa na washindi wa michezo ya mpira wa miguu, mbio za mbataa na kula maandazi ambao ni wanachama wa Jumuia kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa akili Pemba, pamoja na waalimu, maara baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya miaka 24 ya ZSLSC yaliofanyika uwanja wa Gombani Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.