Habari za Punde

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Azindua Umoja wa Madrasa Chumbuni.

Ustadh akitowa maelezo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jumuiya za Umoja wa Madrasa Jimbo la Chumbuni Unguja, Jumla ya Madrasa 45 kati Jimbo la Chumbuni zimeunda Umoja huo. ili kuwezesha kuendekleza Elimu ya Quran kwa Watoto wa Jimbo hilo. uzinduzi huo umefanyika katika Madrasa ya Masumbani. 
Waheshimiwa wakiitikia dua kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya uzinduzi wa Umoja wa Madrasa Jimbo la Chumbuni Zanzibar. 
Viongozi wa Madrasa 45 za Jimbo la Chumbuni Zanzibar wakiitikia dua ikisomwa na mmoja wa Maustadh hao kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya Uzinduzi na kukabidhiwa misahafu na Mhe Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Mhe Ussi Salum Pondeza (AMJAD)
 Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Miraji akitowa nasaha zake kwa Viongozin wa Madrasa za Jimbo la Chumbuni wakati wa uzinduzi huo. uliofanyika katika Madrasa ya Masumbani Chumbuni.
Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe Ali Salum akizungumza wakati wa hafla hiyo na kuchangia Umuoja huo wa Madrasa shilingi laki moja na hamsini ili kuweza kuazia Umoja huo kwa shughuli zake kukuza Madrasa zao.
Viongozi wa Madrasa za Chumbuni wakiwa katika ukumbi wa madrasa ya masumbani wakifuatilia hafla hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza (AMJAD) akimkabidhi fedha zilizotolewa na Mhe Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani Mhe Ali Salum ikiwa mchango wake kwa Umoja huo. 
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza (AMJAD) akizungumza na Viongozi wa Umoja wa Madrasa za Jimbo lake wakati wa uzinduzin huo uliojumuisha Madrasa 45 za Jimbo hilo.
Mbunge wa Chumbuni Mhe Ussi Salum Pondeza (AMJAD) akizungumza na Viongozi wa madrasa wakati wa hafla ya uzinduzi wa madrasa hizo na kuwataka kutowa elimu ya Dini kwa watoto wa jimbo hilo na kuwataka umoja huo uwe ni chachu ya kupata elimu ya dini kwa wananchi wa jimbo la chumbuni Zanzibar. 
Viongozi wa Umoja wa Madrasa Jimbo la Chumbuni wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo hilo wakati akitowa nasaha zake katika hafla ya Uzinduzi huo.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza (AMJAD) akimkabidhi msaada wa Mashafu Mwenyekiti wa Umoja huo kwa ajili ya matumizi ya Madrasa za Jimbo hilo zilizounda umoja wao na kujumuisha Madrasa 45 jimbo ni hapo
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza (AMJAD) akizungumza na Mwenyekiti wa Umoja huo wa Madrasa za Jimbo la Chumbuni kushoto Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Mhe Miraji.

Mwenyekiti wa Umoja wa Madrasa Chumbuni akimkabidhi Msahafu Mbunge Mhe Ussi Pondeza (AMJAD) ili kwenda kuusoma wakati akiwa nyumbani. 
Mwenyekiti wa Umoja wa Madrasa Chumbuni akimkabidhi Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Miraji ili kwenda kuusoma wakati akiwa nyumbani.
Mwenyekiti wa Umoja wa Madrasa Chumbuni akimkabidhi Msahafu Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani Mhe Ali Salum. ili kwenda kuusoma wakati akiwa nyumbani.
Waheshimiwa wakiwa na misahafu yao waliokabidhiwa kwa ajili ya kwenda kuisoma wakati wakiwa nyumbani ili kupata elimu ya Dini.wa kwanza Mhe Ussi Pondeza. Mhe Miraj, na Mhe Ali Salum.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.